News Alert!! MWANDISHI WA HABARI TANZANIA APIGWA VIBAYA NA POLISI,AVUNJWA MIGUU
الاثنين, يونيو 29, 2015
Mwandishi wa Habari kwa jina Omar Ali mzaliwa wa Mkoani Kangani kisiwani Pemba, mida ya asubuhi ameshambuliwa na kupigwa vibaya sana na jeshi la Polisi Zanzibar na kutupwa maeneo ya Maisara mjini Zanzibar.
Mwandishi huyu alikuwa anachukua habari kutoka kituo cha uandikishaji dafatari la kudumu maeneo ya Migombani Zanzibar na polisi hao inasadikiwa walisema ni mwandishi wa Chama cha Wananchi CUF na ndipo walipomshika na kuanza kumpiga vibaya sana na kumvunja miguu kama anavyoonekana kwenye picha akiwa hospital mahutui miguu ikiwa imevujika.
Ikumbukwe: Matukio haya yanakuja baada ya wananchi wa Zanzibar kuhakikisha kila kituo hawezi kuandikishwa mtu ambaye hahusiki kama ambavyo tumeona na kuskia kupitia vyanzo mbali mbali mpango wa CCM kupeleka mamluki visiwani Zanzibar kujiandikisha kwaajili ya kukiokoa Chama cha Mapinduzi hasa Zanzibar ambako kuna kila dalili kungoka madarakani Oktoba mwaka huu.
Chanzo:http://www.udakuspecially.com
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin