News Alert!! NDEGE YA KIJESHI YAANGUKA KWENYE NYUMBA YA MTU YAUA WATU 100
Tuesday, June 30, 2015
Takriban watu 100 wameuawa baada ya ndege ya uchukuzi wa kijeshi ya Indonesia kuanguka mapema leo katika maeneo yenye makazi ya watu huko Medan Sumatra.
Maafisa wa kijeshi wanasema kuwa tayari miili 49 imepatikana katika eneo la ajali. Maafisa wa kijeshi nchini Indonesia, wanasema kwamba ndege hiyo ya uchukuzi ya majeshi ya taifa hilo, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa angani.
Ndege hiyo iliharibu kabisa nyumba ambayo iliangukia katika mji wa Medan, kaskazini mwa jimbo la Sumatra.
Picha za runinga na kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha moto unatoka kwenye mabaki ya ndege hiyo.
Msemaji wa jeshi la angani alisema kuwa rubani alikuwa ameomba kurejea katika uwanja wa kambi ya kijeshi kwa sababu ya matatizo ya kimitambo.
Via>>BBC
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin