Baada ya kufungwa mfululizo kwa timu ya Taifa, Taifa Stars hatimaye kocha mkuu wa timu hiyo Maart Nooij ametimuliwa kazi ya kuendelea kukinoa kikosi hicho.
Kamati ya utendaji ya Shirikisho la soka Tanzania TFF
katika kikao chake kilichokaa jana usiku kimefikia uamuzi huo wa
kumsimamisha kazi kocha huyo kuanzaia leo June 21 pamoja na kuvunja
benchi la ufundi la timu hiyo.
TFF imeahidi kutangaza wakati wowote benchi jipya la ufundi la timu hiyo.
Stars iliambulia kipigo cha mabao 3-0
dhidi ya Uganda jana katika uwanja wa Amaan ikiwa ni mechi ya kwanza ya
kufuzu mashindano ya CHAN 2016 yatakayofanyika Rwanda.
Social Plugin