Ng’ombe
zaidi ya 800 waliokuwa wakisafirishwa kwenda nchi jirani ya Kenya
kupitia mpaka wa Sirari wamekamatwa na mkurugenzi wa halmashauri ya
wilaya ya Tarime baada ya wafanyabiashara watano kugoma kulipa ushuru wa
shilingi elfu tano kwa kila Ng’ombe mmoja.
Wafanyabiashara hao waligoma kutoa ushuru huo kwa madai kuwa ni kinyume na waraka wa katibu mkuu wa wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi unaowataka wafanyabiashara wenye vibali vya kusafirisha mifugo nje ya nchi kutobughudhiwa mahali popote.
Wafanyabiashara hao waligoma kutoa ushuru huo kwa madai kuwa ni kinyume na waraka wa katibu mkuu wa wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi unaowataka wafanyabiashara wenye vibali vya kusafirisha mifugo nje ya nchi kutobughudhiwa mahali popote.
Waraka huo wa Aprili 9 mwaka 2014 unaeleza kuwa mfanyabiashara wa
mifugo mwenye leseni ya kitaifa inayomruhusu kununua na kusafirisha
mifugo kwenda nchi ya jirani anapaswa kulipa ushuru wa shilingi 20,000
kwa kila Ng’ombe, huku Mbuzi na Kondoo wakitakiwa kulipiwa shilingi
5,000 na baada ya malipo hayo mfanyabiashara wa mifugo hapaswi tena
kulipa ushuru au kuchangia huduma nyingine.
Wakizungumza katika eneo la mpaka wa Sirari wilayani Tarime
baadhi wafanyabiashara hao wamelalamikia hali hiyo na kudai kuwa inaweza
kusababisha baadhi ya watu wasio waaminifu kuanza kutumia njia za panya
katika kuvusha mifugo yao nje ya nchi kwa lengo la kuepuka usumbufu wa
kutozwa ushuru mara mbili.
Kwa upande wake mkaguzi wa mifugo wa wizara ya maendeleo ya mifugo
na uvuvi Bonaventura Tesha ameeleza kanuni za udhibiti wa usafirishaji
wa mifugo zinavyotakiwa kutekelezwa na wafanyabiashara wanaosafirisha
mifugo nje ya nchi.
Akijibu malalamiko ya wafanyabiashara hao wanaopinga kutozwa ushuru
mara mbili, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tarime Amos Sagara
amesema kazi ya mawakala walioteuliwa na halmashauri hiyo ni kuhakikisha
ushuru wa Ng’ombe unalipwa kabla ya mfanyabiashara kusafirisha mifugo
nje ya nchi na aina yoyote ile ya ukwepaji haitavulimiwa.
Via>>ITV
Social Plugin