NIMEKULETEA PICHA NYINGI KUTOKA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA CHADEMA MJINI SHINYANGA
Sunday, June 14, 2015
Hapa ni katika eneo la Ngokolo Mitumbani mjini Shinyanga
ambako leo jioni kumefanyika mkutano mkubwa wa Chadema/UKAWA ukiongozwa na mwenyekiti
wa Baraza la Vijana(BAVICHA) Chadema Taifa PatrobasKatambi na viongozi mbalimbali wa BAVICHA
taifa.Lengo la mkutano uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Shinyanga ilikuwa
ni kutoa elimu ya uraia-picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema katika wilaya ya Shinyanga mjini Samson akizungumza katika mkutano wakati wa kukaribisha viongozi wa BAVICHA taifa katika mkutano wao uliofanyika katika kata ya Ngokolo mjini Shinyanga.Pamoja na mambo mengine alieleza kutoridhishwa na wabunge wa CCM huku akisisitiza kuwa endapo Gaki ama Stephen Masele watapitishwa kugombea yuko tayari kupambana nao
Meza kuu wakiwa eneo la mkutano
Kushoto ni Mwenyekiti wa BAVICHA mkoa wa Iringa akizungumza katika mkutano ho wa hadhara
Meza kuu wakiwa eneo la mkutano
Wakazi wa Shinyanga wakifuatilia mkutano huo
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la mkutano
Msemaji wa BAVICHA Elius Julius akizungumza na wakazi wa Shinyanga
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio
Katibu BAVICHA taifa Mwita Julius akizungumza katika mkutano huo ambapo alieleza kukerwa na utitiri wa wanaccm kuwania urais hali ambayo alisema inaonesha ni kiasi wasivyoaminiana na kuwa na tamaa ya kutafuna pesa za wananchi
Hapa siyo sokoni bali ni katika eneo la mkutano
Tunafuatilia mkutano......
Mwenyekiti
wa Baraza la Vijana Chadema Taifa Patrobas
Katambi akiwa na Katibu BAVICHA taifa Mwita Julius
Wananchi wanafuatilia kinachoendelea kwenye mkutano
Kulia ni Naibu
katibu mkuu wa Baraza la Vijana Zanzibar Omary Nassoro akimkaribisha jukwaani mwenyekiti wa BAVICHA taifa Patrobas Katambi ili azungumze na wakazi wa Shinyanga.
Awali Naibu
katibu mkuu wa Baraza la Vijana Zanzibar Omary Nassoro aliwatahadharisha
watanzania wakati wa uchaguzi mkuu ujao kuchagua viongozi wanaowafaa badala ya kuchagua viongozi wanaojali
maslahi yao binafsi.
Mwenyekiti
wa Baraza la Vijana Chadema Taifa PatrobasKatambi akizungumza katika mkutano huo ambapo
amewataka wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kuungana pamoja na kuepuka migogoro ili
kuiondoa madarakani serikali ya Chama Cha Mapinduzi badala ya kugombania
madaraka ndani ya chama.
Patrobas Katambi alieleza pia nia yake ya kuwania ubunge katika jimbo la Shinyanga mjini na endapo jina lake likikatwa yupo tayari kumpa ushirikiano mgombea wa Chadema kwani CHADEMA inaamini katika umoja na mshikamano
Mwenyekiti
huyo wa BAVICHA pia amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika
daftari la kudumu la wapiga kura kwani ndiyo tiketi itakayotumika kuondoa
viongozi wasiofaa kwa wananchi.
Mtangaza nia kuwania ubunge katika jimbo la Shinyanga mjini Francis Kasiri akiwasalimia wakazi wa Shinyanga
Mwenyekiti
wa Baraza la Vijana Chadema Taifa PatrobasKatambi,ambaye pia ni mtangaza nia kuwania jimbo la Shinyanga akiwa amebebwa na wakazi wa Shinyanga baada ya mkutano kuisha
Wakazi wa Shinyanga wakitafakari jambo baada ya mkutano wa CHADEMA kumalizika. Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin