Wanaccm wakipanda gari la taka la mji wa Geita-Picha zote na Victor Bariety-Malunde1 blog Geita |
Msafara wa Kinana ukiingia Geita
Baiskeli zikizosombwa na magari ya taka toka ofisi ya ccm mkoa wa Geita |
Baiskeli zilizosombwa na magari ya taka toka ofisi ya ccm mkoa zikiwa zimerundikwa uwanja wa Nyankumbu Geita
Kinana akiwasili uwanja wa nyankumbu Geita kuhutubia wananchi |
Kinana akiwa amemkaba koo mkurugenzi wa GEWASA Injia Clemence Chagu awaelezi wananchi ni lini maji yataanza kutoka mjini hapo |
Kinana akiwa amemkaba koo mkurugenzi wa GEWASA Injinia Clemence Chagu awaelezi wananchi ni lini maji yataanza kutoka mjini hapo |
Wanaccm wakipanda gari la taka la mji wa Geita |
Wakijiandaa kupanda gari la taka |
Msafara wa katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi(CCM),Abdulrahman
Kinana Juni 20 mwaka huu ulitumia magari kadhaa ya serikali katika Wilaya tano
na majimbo sita ya uchaguzi kwenye mkoa wa Geita,huku maroli yanayotumika
kubeba taka kwenye halmashauri ya mji wa Geita yakitumika kusomba wanachama wa
chama hicho kuwatoa nje ya mji wa Geita ili kujaza mkutano wake.
Mbali na magari hayo, wakuu wa wilaya waliokuwa wameshiriki msafara wa katibu mkuu huyo wa CCM, walitumia magari yao ya kazi huku wakivalia sare za chama hicho.
Baadhi ya magari ya serikali yaliyotumika kupamba msafara wa Kinana aliyekuwa kwenye gari namba, T170 BHT Landcruser,ambayo hutumiwa na wakuu wa idara mbalimbali za Serikali na kufanya msululu kuwa mrefu kana kwamba ni ugeni wa waziri mkuu Mizengo Pinda,ni pamoja na DFP 8525 Toyota Hillux(TAMISEMI MKOA),STL 736 Toyota Landcuruser(NSSF MKOA),na DFP 8518 Toyota Hillux(IDARA YA UKAGUZI).
Mengine ni STK 6803 Toyota 4WD,DFP 674 Nissan,SU
37541Nissan Patrol,SM 11013 Landcruser Prado,DFP 4604 Toyota 4WD,pamoja na DFP
9765 Toyota Hillux huku mengine ya wakuu wa idara mbalimbali za serikali,
yalitumika na kuwekwa namba binafsi.
“Tunashindwa kuelewa hii ni ziara ya chama au ya kiserikali?maana hata msafara wa waziri mkuu Pinda haufikii hapa huku si nikuharibu fedha za serikali?we unadhani kwa haya magari yanavyokunywa mafuta ni kiasi gani cha pesa kimetumika?we subiri oktoba tunakwenda kuderete CCM’’…walisikika baadhi ya watu walioshuhudia msafara huo wakiteta.
Msafara huo ulikuwa ukitokea kuzindua mradi wa maji uliopo jirani na ofisi za halmashauri ya wilaya ya Geita kuelekea katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Geita(GEDECO),kabla ya kuelekea kwenye uwanja wa Nyankumbu ambako Kinana alipata fursa ya kuhutubia wananchi.

Hata hivyo wakati hayo yakiendelea,Malunde1 blog ilishuhudia
baadhi ya magari(Maroli)ya halmashauri ya mji wa Geita ambayo hutumika kubeba
taka zinazorundikwa kwenye madampo maeneo mbalimbali ya mji wa
Geita,yakipishana kwa kusomba watu(wafuasi wa chama hicho), kuwatoa maeneo
mbalimbali nje ya mji wa Geita na kuwapeleka katika uwanja wa nyankumbu ambako
mkutano wa hadhara wa Kinana ulifanyika.
Baadhi ya magari hayo ni pamoja na yenye namba za
usajili SM 10690 na SM 10691 yote aina ya FAW na baada ya kazi hiyo,yalirudi
katika ofisi za chama hicho mkoa na kuanza kusomba baiskel 170 na kuzipeleka
kwenye uwanja huo ambazo zimetolewa na mbunge Vicky Kamatta kwa ajili ya
kinamama wa UWT kwenye mkoa huo.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Emilly Kasagala
alitetea hatua hiyo akisema sio kosa kwa kuwa Kinana anakagua utekelezaji wa
ilani ya CCM.
Kasagala, alikiri kutumika kwa magari hayo ya serikali na kusema kuwa viongozi hao waliyatumia kumpokea na baadhi yao waliambatana naye katika ziara hiyo kwa kuwa mbali na kuwa katibu mkuu wa CCM ziara hiyo mbali na kuimarisha chama pia anakagua utekelezaji wa ilani ya CCM.
“Huyu ni katibu mkuu,licha ya kuwa kiongozi mkuu na mtendaji wa chama cha mapinduzi amekuja pia kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM,sasa ma-DC walikuja kama makada na viongozi wa serikali kumpokea Kinana. Kama kuna mkuu wa wilaya alivaa shati la CCM alivaa kwa sababu ya mapenzi yake kwa chama lakini sisi wataalamu nadhani umeona hakuna aliyekuwa amevalia sare za chama,” alifafanua Kasagala kwa kujiamini.

"Makosa ni kiongozi wa serikali kufanya kazi za
chama na sioni kama kuna kiongozi wa serikali ambaye alifanya kazi za
chama,lakini sababu zilizopelekea magari ya serikali kupamba msafara wake kubwa
ni hiyo kwamba alikuwa anakagua utekelezaji wa ilani ya CCM na watekelezaji wa
ilani hiyo ni sisi na ndiyo maana kila eneo alilofika alikabidhiwa taarifa ya
chama na ya serikali"alisema
Aidha kwa mjibu wa Katibu wa siasa na uenezi wa Chama hicho,Nape Nnauye akiwa Mkoani Geita,Kinana ametembea umbali wa kilometa 1680 ambapo aliweza kufika kwenye wilaya zote tano za mkoa wa Geita na majimbo sita ya uchaguzi.

Kwenye maeneo yote hayo,Kinana alifanya mikutano
sita ya ndani na 60 ya nje,alikagua miradi 53 ya maendeleo kati yake 5 ya chama
pamoja na kuingiza wanachama wapya wa CCM 6816 kati yake 640 wakitokea vyama
vya upinzani.
Akihutubia wananchi wa Geita,Kinana aliwataka
watendaji wa serikali kuacha kukaa maofisini na badala yake wajenge mazoea ya
kuwatembelea wananchi ili kujua changamoto zinazowakabili.
Na Victor Bariety- Malunde1 blog Geita
Social Plugin