KIONGOZI mkuu wa chama cha ACT WAZALENDO Zitto Zuberi Kabwe na Mwenyekiti wake Anna Ngwira kwa nyakati tofauti wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa hadi kupelekea kukatisha hotuba zao.
Wakwanza kuzomewa kwenye mkutano huo uliofanyika katika uwanja wa standi ya zamani ya mjini Geita alikuwa mwenyekiti wa chama hicho baada ya kupanda jukwaani kisha kuanza kuwahutubia wananchi akielezea sera za chama chake bila kujali muda.
Ngwira alikuwa akielezea sababu ya chama hicho kuzindua azimio la Tabora lakini hakuweza kumalizia hotuba yake hiyo baada ya wananchi kulipuka wakimtaka apishe jukwaa hilo ili wasikilize sera za Zitto.
‘’Tokaaaa…huna jipya wewe tunamtaka Zitto………….walisikika baadhi ya wananchi
wakipiga yowee kupinga hotuba ya mwenyeakiti huyo’’
‘’Geita hoyeeeeeeeeeee….Geita hoyeeeeeeeeeeeeeee…alisema Kabwe huku akiitikiwa na wananchi kisha kuanza kuhutubia wananchi ambapo alizungumzia jinsi alivyowapigania wananchi Wa mkoa wa Geita hususani katika Sekta ya madini wakati akiwa mbunge.
Mbali na hilo aliwataka wananchi wa Geita kukipokea chama hicho na kuhakikisha kinapata wawakilishi wa ngazi ya Udiwani,na Ubunge kwa madai kuwa ndicho chama pekee kilichopo kwa ajili ya kumkomboa mtanzania.
ACHAFUA HALI YA HEWA
Hata hivyo mbali na utulivu wa hali ya juu uliokuwepo kwenye mkutano huo ukimsikiliza Kabwe kwa makini,hali hiyo ilibadirika ghafla baada ya yeye(Kabwe)kuanza kukinanga chama chake cha zamani.
‘’Wengi mpo hapa kwa ajili ya kusubiri nieleze mgogoro wangu na chama changu cha zamani,mie sipo hapa kwa ajili hiyo maana kilichonileta hapa ni kutangaza sera za chama changu’’
‘’Ndiyo maana mkutano umetulia kwa ajili ya sera nzuri ambazo ninaendelea kuwaeleza,vyama vingine ni matusi na hapa mngekuwa mnacheka kwa ajili ya matusi yao’’
Najua mmelishwa sumu nyingi sana kuhusu Kabwe…ninachotaka kusema ng’ombe si mnamfahamu?kwenye ng’ombe kinachotikisika ni mkia na siyo ng’ombe…hivyo mimi ni Ng’ombe na kile chama changu cha Zamani ni mkia ndiyo maana kinatikisika lakini mimi kama ng’ombe hawazi kunitikisa’’alisema Kabwe jambo ambalo liliibua zogo na wananchi kuzomea huku wakimwita yuda.
Zomeazomea dhidi ya Kabwe ilitawala katika kipindi chote alichokuwa jukwaani huku viongozi wa chama wakihaha kuwazuia wananchi wasizomee bila mafanikio.
Kufuatia hali hiyo,ilimlazimu Kabwe kushuka jukwani na baadaye umati wa wananchi ulisimama kando ya barabara kuu kisha kunyoosha vidole viwili na kila alipopita alikutana na vidole viwili vilivyoambatana na zomeazomea.
Baaadaye Kabwe alikwenda kuweka jiwe la msingi katika ofisi yao iliyopo mtaa wa nyerere road kabla ya kuanza safari kuelekea wilaya ya Biharamlo mkoani Kagera.
Na Victor Bariety-Malunde1 blog Geita
Social Plugin