Mwandishi wa habari hizi amefika eneo la Mburahati kwa Madoto zilipo ofisi hizo za
Chadema na kukuta upande wa mbele wa ofisi hiyon ukiwa umebomolewa na
baadhi ya vitu kuvunjwa huku uongozi wa ofisi hiyo ya Chadema
ukielekezea lawama kwa serikali ya mtaa wa Mburahati kwa madoto kwa
kuhusika na ubomoaji huo pasipo kufuata taratibu za ubomoaji.
Akijibu tuhuma hizo afisa mtendaji wa kata hiyo ya Mburahati hiyo
Bi.Scholastica Matinde amesema sheria hairuhusu kwa chama chochote cha
siasa kuweka ofisi kwenye maeneo ya masoko kama ambavyo chama hicho cha
Chadema kilivyofanya.
Via>>ITV
Social Plugin