|
Mtangaza
nia kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao Charles Makongoro Nyerere
leo amekamilisha ziara ya kutafuta wadhamini
mikoani.Ziara yake ameikamilisha katika mkoa wa Shinyanga.Katika hotuba yake ya kukamilisha ziara yake,Makongoro Nyerere amekemea vitendo vya mafisadi aliodai hawazidi 20,anaowafahamu sura,majina na tabia zao ambao wamekuwa kikwazo hata kwa rais Jakaya Mrisho Kikwete,aliodai kuwa wengi ni marafiki zake na rais.Mwandishi wetu Kadama Malunde,ametuletea picha na HOTUBA NZITO YA MAKONGORO akizungumzia ufisadi ndani ya CCM huku akimtaja Mheshimiwa Edward Lowassa kuwa hafai kuwa rais wa Tanzania(HOTUBA IKO MWISHONI MWA PICHA HAPA CHINI
|
|
Hapa ni katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi za Wilaya ya Shinyanga mjini,mkoa wa Shinyanga.Aliyesimama ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid akimkaribisha mheshimiwa Makongoro Nyerere(ambaye ni mtoto wa baba wa taifa Julius Kambarage Nyerere),aliyefika leo Shinyanga kuchukua fomu ya majina ya wadhamini 30 kama alivyohitaji ili agombee urais katija uchaguzi mkuu 2015. | | | |
|
|
Mtia nia ya urais Makongoro Nyerere akiwasalimia wadhamini wake kutoka mkoa wa Shinyanga waliojitokeza kumpokea katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga |
|
Makongoro akizungumza wakati wa kuchukua fomu ya majina 30 ya wadhamini kutoka mkoa wa mwisho kati ya mikoa yote aliyozunguka kusaka wadhamini |
|
Makongoro Nyerere wakati wa kuchukua wadhamini wake 30 katika
ofisi za wilaya ya Shinyanga mjini mkoani Shinyanga kama alivyohitaji ambapo
amesema CCM inapoteza mwelekeo kutokana na baadhi ya wanachama wake kuendekeza
ufisadi.
|
|
Pichani ni wadhamini wake kutoka Shinyanga-Makongoro Nyerere amewataka wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama
Cha Mapinduzi kuhakikisha wanatenda haki kupitisha jina la mgombea atakayerudisha
heshima ya CCM iliyopotea na kwamba endapo CCM itakosea uteuzi wa kumsimika
mgombea makini nchi itakwenda na upinzani.
|
|
Makongoro amesema watanzania wanaendelea kuwa maskini kutokana na tabia mbaya ya baadhi ya mafisadi ambao wamekuwa wakimsumbua rais Jakaya Kikwete na kuonekana hafanyi kazi kumbe tatizo ni hao marafiki zake |
|
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura(kulia) akikabidhi fomu
ya majina ya wadhamini wa mtia nia ya urais Makongoro Nyerere |
Makongoro Nyerere akipokea fomu yenye majina ya wadhamini 30 kutoka mkoa wa Shinyanga
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura akikabidhi fomu ya majina ya wadhamini wa mtia nia ya urais Makongoro Nyerere
|
Makongoro Nyerere akishikana mkono na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid |
|
Makongoro Nyerere akionesha mkoba uliobeba Fomu zake baada ya kukamilisha zoezi la kupata wadhamini na kuelekea Dodoma kwa ajili ya kukabidhi fomu hizo makao makuu na kubiri jina lake lipitishwe na kikao cha halmashauri kuu ya CCM Julai,12 mwaka huu |
Charles Makongoro Nyerere amesema baada ya kazi ya kutafuta wadhamini chini ya Chama Cha Mapinduzi bila kuvunja utaratibu na kanuni kwa mikoa
mbalimbali kutoka Tanzania bara na visiwani mwishowe amemaliza kwa wakati na kesho tarehe 19/06/2015 atarudisha
fomu pale makao makuu ya chama Dodoma.
|
Picha ya pamoja,Makongoro Nyerere na wadhamini wake kutoka mkoa wa Shinyanga juu ya jengo la CCM wilaya ya Shinyanga mjini |
|
Makongoro Nyerere na wadhamini wake kutoka mkoa wa Shinyanga juu ya jengo la CCM wilaya ya Shinyanga mjini |
|
HAPA NI NJE NYUMBANI KWA HAYATI MUFTI ISSA SHAABAN SIMBA KATIKA MTAA WA MAJENGO MJINI SHINYANGA.Akiwa
mkoani Shinyanga Makongoro amekwenda kumpa mkono wa pole mjane wa aliyekuwa
mufti mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaaban bin Simba ,Mwanagoso nyumbani kwake
katika mtaa wa Majengo mjini Shinyanga na kutoa ubani.Pichani ni Makongoro Nyerere akishikana mkono na Shehe wa wilaya ya Shinyanga Sudy Kategire |
|
Makongoro Nyerere akizungumza jambo na kaka yake na hayati Mufti Simba,Ramadhan Simba alipofika kuwapa mkono wa pole |
|
Makongoro Nyerere akiwa nyumbani kwa hayati Mufti Simba |
|
Makongoro akimpa mkono wa pole mjane wa aliyekuwa
mufti mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaaban bin Simba ,Mwanagoso nyumbani kwake
katika mtaa wa Majengo mjini Shinyanga pamoja na kutoa ubani |
|
Makongoro Nyerere akiwa ndani ya nyumba ya hayati Mufti Simba |
Makongoro Nyerere akimpa mkono wa pole mjukuu wa hayati Mufti Simba
IFUATAYO NI HOTUBA NZITO ALIYOITOA MAKONGORO NYERERE WAKATI AKICHUKUA WADHAMINI WAKE MKOANI SHINYANGA
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin