Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe. Jenista
Mhagama (mwenye nguo nyekundu) akimfariji Mwenyekiti wa Bunge Bi.
Lediana Mng’ong’o mara baada ya bunge kuahirishwa kufuatia kifo cha
aliyekuwa Mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa. Kulia ni Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Utawala Bora Bi. Mary Nagu na kushoto ni wabunge James
Mbatia na Goodluck Ole Medeye.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anjela Kairuki
(kushoto) akitoka nje ya ukumbi wa bunge akiwa ameambatana na wabunge
Bi. Mary Mwanjelwa na Rita Kabati baada ya bunge hilo kuahirishwa
kufuatia kifo cha Mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa.
Aliyekuwa
mbunge wa jimbo la Ukonga marehemu Bi. Eugen Mwaiposa ambaye amefariki
usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mjini Dodoma. Taarifa za kifo chake
zimetangazwa wakati bunge likiendelea na mjadala wa bajeti ya wizara ya
afya hivyo kupelekea bunge hilo kuahirishwa hadi tarehe 4 mwezi huu.
Baadhi ya wabunge wakiwa kwenye hali ya simanzi baada ya kutangazwa kifo cha aliyekuwa mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa kilichotokea usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mjini Dodoma.
Picha kwa hisani ya Michuzi blog
Social Plugin