Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa
Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max,
wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye
Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne
Makinda, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es
Salaam, leo Juni 27, 2015 kwa ajili ya kushiriki shughuli za kuaga mwili
wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akisaini
katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita,
kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa
shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja
vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mke wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete, akisaini
katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita,
kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa
shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja
vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais
Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Makamu wa Dkt. Bilal, wakati walipokuwa
katika shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu
Donald Kelvin Max, zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya
Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais
Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Bilal, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
na baadhi ya Viongozi wakijumuika na waombolezaji katika shughuli za
kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max,
leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais
Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin
Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015
kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais
Jakaya Kikwete, akiifariji familia ya marehemu Max, wakati wa shughuli
za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya
Karimjee jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiifariji familia ya marehemu Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili
zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar
es Salaam. Picha na OMR.
Social Plugin