Mwenyekiti
wa umoja wa vyama vinavyounda UKAWA nchini na mwenyekiti wa chama cha
wananchi (CUF) Mhe. Prof Ibrahim Haruna Lipumba ametangaza nia ya
kupeperusha bendera ya ukawa kwa kugombea urais, katika uchaguzi mkuu
ujao Oktoba ili kupewa ridhaa na wananchi ya kuiongoza nchi ya Tanzania.
Akiwahutubia umati mkubwa wa wananchi katika viwanja vya Mwananchi
Squer katika mji mdogo wa Urambo mwenyekiti wa UKAWA Ibrahimu Lipumba
amesema kuwa, kama UKAWA utaamua kumpitisha mgombea mwingine atakuwa
tayari kumpigia debe mteule wa UKAWA, lakini malengo yake ya kutaka
kugombea urais, kwalengo la kutafuta haki ya wananchi ambayo imepotea.
Aidha katika hatua nyingine Mhe Prof Ibrahimu Lipumba amewataka
watanzania kutambua kwa changamoto ambazo zinawakabili zikiwa ni
upatikanaji wa haki za kijamii, zitaondolewa na rais ambaye atatoka nje
ya chama cha mapinduzi na si vinginevyo, na kama hawatachagua rais
kutoka nje ya CCM wajue hali ngumu ya maisha itaendelea kuwakabili
kutokana na kutokuwepo na haki.