Rais
Jakaya Kikwete amesema serikali yake itaendeleza mapambano dhidi ya
kundi la watu wasio na utu wanaoua na kuwajeruhi watu wenye UALBINO
nchini kwa madai ya kutafuta utajiri ili kuhakikisha kuwa walemavu hao
wanaishi maisha ya amani kama katiba ya nchi na mikataba ya kimataifa
inavyoelekeza.
Akizungumza ma maelfu ya wananchi waliohudhuria maadhimisho siku
ya watu wenye UALBINO duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Arusha Rais
Kikwete aliyeonyesha kuguswa na ujumbe uliofikishwa na watoto wenye
UALBINO kwa njia ya nyimbo amesema ni kwa kutambua kuwa vitendo hivyo
vimekua vikichochewa na imani za kishirikina serikali yake ililazimika
kupitia upya baadhi ya sheria hususani zile zinazolinda maslahi ya watu
wenye ulemavu.
Maadhimisho hayo yalitanguliwa na dua kutoka kwa viongozi wa dini
ambao wote kwa pamoja wanakemea unyanyasaji unaofanywa dhidi ya walemavu
hao.
Kilio chao kingine cha watu wenye ualbino upatikanaji wa huduma ya afya stahiki.
Katika hilo mwakilishi mkazi wa umoja wa mataifa nchini Alvaro
Rodrguez anasema wanashirikiana na serikali kuhakikisha kuwa kundi hilo
linapata huduma huku wizara ya afya ikisema tayari imeshajenga mazingira
mazuri ya upatikanaji wa mafuta ya kuzuia mionzi ya jua inayosababisha
saratani ya ngozi.
Via>>ITV
Social Plugin