Nyuki waliwahi kuibua stoty kubwa baada ya kuvamia ndege aina ya Boeing 757 mwaka 1996 ambapo
ndani ya dakika tano baada ya kuondoka ilikuwa ishu baada ya
kugundulika kwamba sehemu ambayo inaonesha mwendokasi wa ndege imezibwa
na kundi la nyuki.
Leo
kuna hii stori kutoka Uingereza inayohusisha nyuki na ndege.. abiria
walilazimika kukaa kwa masaa mawili baada ya nyuki kuingia kwenye moja
ya mitambo ya injini za ndege, haikuwa salama sana ndege hiyo kuanza
safari wakati kuna hali hiyo.
Ndege hiyo inayoitwa Flybe yenye namba BE384 ilikuwa ikitoka Southampton kuelekea Dublin.
Shirika linalomiliki ndege hiyo limesema
isingekuwa salama sana wao kuendelea na safari wakati nyuki wako ndani
ya injini, ilibidi watolewe na baadae safari yao ikaendelea..
Social Plugin