Mwalimu mmoja mkuu amekiri kufanya ngono na wavulana wawili wenye umri mdogo.
Anne
Lakey, mwenye umri wa miaka 55, kutoka eneo la Stanley, katika kaunti
ya Durham, amekanusha makosa 13 dhidi yake ya kufanya matendo ya aibu
kwa kushikashika sehemu za siri wavulana wawili miaka ya themanini.
Lakini jaji katika mahakama ya Teesside Crown, alimpata na hatia ya makosa hayo yote baada ya kesi iliyochukua majuma mawili.
Mahakama
ilisikiza ushahidi wa namna alivyokuwa akitenda matendo hayo ya kuudhi
na aibu katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
Atahukumiwa jela Jumatano wiki hii.
Mahakama
iliambiwa kuwa baadhi ya makosa yalifanyika pale Lakey alipokuwa
mwalimu wa kufundisha somo la historia akiwa na umri wa miaka 20.
Lakey,
ametajwa na waendesha mashtaka kama "mnyama wa ngono", alimlenga
mvulana wa miaka 15 na waathiriwa wengine wawili wenye umri wa kati ya
miaka 13 au 14.
Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, mmoja wa
waathiriwa aliwaambia majaji kuwa mama huyo wa mtoto mmoja alimuondolea
ubikra pale alipomtaka amtizame alipokuwa akioga.
Lakey alifanya
kazi yake ya ualimu kwa ushindi mkubwa kwani alisifiwa mno kwa
kufaulisha Shule hiyo iliyokuwa imedorora kielimu na kuifanya mojawepo
ya shule iliyopata mafanikio makubwa.
Lakini mnamo mwaka 2012,
mojawepo wa waathiriwa alituma ujumbe kwa njia ya barua pepe hadi
shuleni humo, iliyosababishwa afutwe kazi na kisha polisi
wakafahamishwa.
via>>BBC
Social Plugin