Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SIMBA AFUNGUA DIRISHA LA GARI,AUA MTALII AKISHANGAA WANYAMA

animalplIX-15

Vyombo vikubwa vya habari vimeripoti sana hii ishu leo June 02 2015, unaweza ukaamua kufungua kioo ili uone vizuri wanyama wakati uko mbugani unatalii, hii sio salama sana kwa vile kwenye hifadhi kuna wanyama wengine wakali kama simba ambao wanaweza kufanya chochote kibaya wakipata nafasi.

Niliwahi kukuwekea kipande cha video kilichoonesha simba wakifungua mlango wa gari ya watu waliokuwa wakitalii mbugani, lakini simba hakuwadhuru.. Hii nyingine imetokea South Africa, kwenye hifadhi ya wanyama ambayo iko kama umbali wa Kilometa 30 hivi toka Johannesburg.

Mwanamke alikuwa ndani ya gari akiendelea kutalii ndani ya Lion Park, akatokea simba jike mmoja, akavamia kwenye gari kupitia kwenye dirisha la gari na kumshambulia mwanamke ambaye alifariki kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata.

Askari wa hifadhi waliwahi na kuwafukuza simba lakini mwanamke alifariki kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata huku mwanaume aliyekuwa akiendesha gari hiyo akiendelea kupata matibabu baada ya kujeruhiwa pia.. tukio la mtu kufariki kutokana na kujeruhiwa na simba hii ni mara ya tatu ndani ya kipindi cha miezi minne ndani ya hifadhi hiyo.


Hii ni video ya simba alivyofungua mlango wa gari.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com