Mganga wa
Hospitali ya Wilaya ya Geita ambaye hakujulikana jina lake mara moja akiwa anampa
huduma mwananchi wa kijiji cha Rwamgasa Paulo Mtalima ambaye ni mtia nia jimbo la Busanda kupitia CHADEMA baada ya kukatwa
mapanga na watu wasiojulikana -Picha na
Valence Robert Malunde1 blog Geita.
Mtangaza nia kuwania ubunge katika jimbo la Busanda Wilayani Geita Mkoani Geita kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Paulo
Mtalima (30) mkazi wa kata ya Rwamgasa amekatwa mapanga na watu wasiojulikana
wakati akienda nyumbani kwake.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana majira ya saa mbili
na nusu usiku wakati mtia nia huyo alipokuwa matembezini kuelekea nyumbani
kwake.
Baadhi ya mashuhuda waliomsaidia mtu huyo walisema walisikia kelele zikipigwa akiomba msaada na mara baada ya kufika
walikuta mtu mmoja ambaye hakujulikana jina lake wala sura yake akiwa anatokomea.
“Mimi nilifika hapa kumpa msaada huyu kama jirani yangu
nilisikia akipiga kelele nilifika na kuona mtua akiwa ameshika panga na anaishilizia
gizani kwahiyo sikuweza kumfahamu”alisema shuhuda wa tukio hilo.
Mke wa mtia nia huyo Sara Mtalima alisema kuwa mme wake hakuwa
na ugomvi na mtu yeyote lakini tangu atangaze nia kupitia Chadema amekuwa
akipewa vitisho kupitia simu yake ya mkononi.
“Mme wangu hajawahi kugombana na mtu yeyote yule na hapa
kijijini anaelewana na kila mtu, lakini
tangu atangaze nia amekuwa akitishiwa kweye simu yake hali iliyomsababisha
mpaka kuogopa kutembea”,alisema Sara.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Geita Adam Sijaona walimpokea majeruhi huyo na kumlaza katika wodi Namba 8 na kwamba hali yake
inaleta matumaini kidogo kutokana na kukatwa mapanga mengi kichwani na kuvuja damu
nyingi.
Kaimu kamanda wa Jeshi la polisi Peter Kakamba alipotafutwa
kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo simu yake ya mkononi iliita bila
kupokelewa.
Na Valence Robert- Malunde1 blog Geita