Familia ya Mwanamuziki Banza Stone imekanusha taarifa zinazozidi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kifo cha msanii Banza Stone.
Akiongea na Malunde1 Blog hivi punde,Kaka wa msanii huyo Jabir Ally Masanja anayepatikana kwa simu namba 0753-786016 amesema kuwa mdogo wake ni mzima,tangu jana atoke hospitali yupo nyumbani kwao Sinza Vatican,hali yake ni nzuri anaendelea vyema na anazungumza.

Jabir amesema tangu jana usiku amepokea simu nyingi sana kuhusu taarifa hizo ikiwa ni pamoja na kupewa pole na watu kufika nyumbani.
Amesema taarifa hizo siyo za kweli kwani Banza Stone ni mzima kabisa.
"Tumepata hizi taarifa za kizushi jana saa tatu usiku,Tumepata usumbufu sana,hatujalala kabisa,ukweli ni kwamba kaka yangu ni mzima,anaongea,nasikitika sana kwanini watu wanazusha taarifa za uongo,sijui kwanini watu wanafanya vitu kama hivi,inasikitisha sana,watu wa mitandao ni vyema wakawa na uhakika wa vitu wanavyopost siyo kukurupuka tu",amesema Jabir.
MSIKILIZE HAPA JABIR AKIZUNGUMZA NA MALUNDE1 BLOG HIVI PUNDE.....
Social Plugin