Timbwili
la aina yake lilizuka mwishoni mwa wiki iliyopita baada njiwa aliyekuwa
amefungwa hirizi na barua iliyokuwa imeandikwa kwa Lugha ya Kiarabu
kuzunguka katika baa zipatazo 26 zilizopo Banana, wilayani Ilala, Dar es
Salaam.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu kutoka eneo hilo, njiwa huyo alizunguka katika
kila baa iliyopo eneo hilo na mwisho alitua jirani ya baa moja.
Kabla
ya kutua katika paa za baa hizo, baadhi ya watu waliokuwa wakipata
kinywaji walisema njiwa huyo alionekana kwa muda mrefu akiwa anaruka na
vitu vyeupe kwenye mbawa zake.
Mmoja
wa wateja katika baa hiyo alisema licha ya kumuona ndege huyo
hawakujali na badala yake walimkamata na kumwondolea hirizi na
karatasi.
Social Plugin