TAZAMA PICHA 30- KOMBE LA MEYA SHINYANGA 2015 LAZINDULIWA,TIMU 18 KUCHUANA,MSHINDI KUONDOKA NA ZAWADI NONO!!

Mashindano ya Kombe la Meya Shinyanga 2015 (Pepsi Meya Cup 2015) yamezinduliwa rasmi leo na mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga.

Mashindano hayo ambayo yameandaliwa na mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam na kudhaminiwa na kampuni ya Vinywaji baridi ya  Pepsi (SBC Tanzania Ltd) yanashirikisha timu 17 za kata zote za manispaa hiyo na timu ya polisi Shinyanga.

Mashindano ya Kombe la Meya Shinyanga yakihusisha mpira wa miguu yataendelea kufanyika hadi tarehe 25,Julai 2015 na yatakuwa yanafanyika siku tatu kwa wiki yaani Ijumaa,Jumamosi na Jumapili.

Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo ataondoka na kitita cha shilingi milioni moja na laki tano,kombe na medali ya dhahabu,wa pili shilingi milioni moja,kombe dogo na medali ya fedha na wa tatu shilingi laki tano,kombe dogo na medali ya shaba.

Malunde1 blog ilikuwepo wakati wa uzinduzi huo,Kadama Malunde,ametuletea picha kutoka eneo la tukio….Tazama hapa chini
Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akizungumza wakati wa ufunguzi wa Pepsi Meya Cup Shinyanga 2015,ambapo alisema lengo la mashindano hayo ya mpira miguu kwa vijana yatakayoshirikisha timu 18 za manispaa ya Shinyanga ni kwa ajili ya burudani,ajira na kusaka vipaji kutoka kwa vijana katika manispaa ya Shinyanga.

Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh alisema mashindano hayo yatakuwa yatafanyika kwa muda wa mwezi mmoja na yatafanyika mara tatu kwa wiki katika viwanja vitatu vya Shycom,Kambarage na Polisi mjini Shinyanga.

Mashindano hayo yameanza leo Juni 26,2015 yatafikia tamati Julai 25,2015

Meza kuu wakiwa eneo la tukio

Meneja mauzo wa Kampuni ya vinywaji baridi Pepsi kanda ya Ziwa Seni Makwaya akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kombe la Meya Shinyanga 2015 ambapo alisema katika mkoa wa Shinyanga ndiyo mara ya kwanza kwa kampuni ya Pepsi kudhamini mshindano ya meya,ingawa huu ni mwaka wa tatu nchini Tanzania tangu waanze kudhamini mashindano ya namna hiyo.

Meneja mauzo  wa kampuni ya vinywaji baridi SBC Tanzania Limited (Pepsi) bwana Promod  Nair akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kombe la meya Shinyanga 2015 ambapo alisema wameamua kudhamini mashindano hayo ili kuinua vipaji kutoka kwa vijana katika manispaa ya Shinyanga.

Meneja mauzo kampuni ya Pepsi mkoa wa Shinyanga bwana Benson Tweve akizungumza katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambapo alizitaka timu za Stand United na Mwadui FC kutumia fursa ya mashindano hayo ya Meya Cup kuchukua vijana wenye vipaji kwa ajili ya kuinua mkoa wa Shinyanga kimichezo.

Mgeni rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kombe la Meya Shinyanga 2015,ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka vijana wa Shinyanga kutumia fursa ya mashindano hayo kuonesha vipaji vyao kwani michezo ni ajira.

Mgeni rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro akikabidhi vifaa vya michezo kwa afisa mtendaji wa kata ya Masekelo yenye Timu ya Masekelo fc iliyocheza mechi ya ufunguzi na Ngokolo fc kutoka kata ya  Ngokolo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza katika mchezo wa mbio za baiskeli  Kulwa Ntyuki uliofanyika mjini Shinyanga wakati wa ufunguzi wa kombe la meya Shinyanga

Mgeni rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro akikabidhi vifaa vya michezo kwa afisa mtendaji wa kata ya Ngokolo



Waamuzi wa mchezo wa ufunguzi wakikagua wachezaji wa timu ya Masekelo fc na Ngokolo fc

Mgeni rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine akikagua timu ya Masekelo fc  kabla ya mechi ya ufunguzi kati ya Masekelo fc na Ngokolo fc haijaanza katika uwanja wa mpira wa Shycom Mjini Shinyanga .

Mgeni rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine akikagua timu ya Ngokolo fc kabla ya mechi ya ufunguzi kati ya Masekelo fc na Ngokolo fc haijaanza katika uwanja wa mpira wa Shycom Mjini Shinyanga

Waamuzi wa mchezo wakiwa uwanjani
Mgeni rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine akizungumza na wachezaji wa timu ya Ngokolo fc  na  Masekelo fc na Ngokolo fc

Mgeni rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro akijiandaa kupiga penati huku meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akiwa golini.

Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akihangaika golini baada ya kufungwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.

Mechi kati ya Masekelo fc na Ngokolo fc ukiendelea ambapo hadi mwisho wa mchezo,Masekelo fc bao 2,na Ngokolo fc bao 2.

Wakazi wa Shinyanga wakishuhudia mechi

Wengine walipaki na baiskeli zao uwanjani kujionea kilichokuwa kinajiri uwanjani

Mchezo unaendelea

Tunafuatilia kinachoendelea....

Wachezaji wa Masekelo fc wakishangilia goli lao la kwanza

Wakazi wa Shinyanga wakiwa juu ya ukuta wakifuatilia mechi

Tunafuatilia mechi......

Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam(mwandaaji wa Kombe la Meya Shinyanga 2015) akiteta jambo na  Meneja mauzo  SBC Tanzania Limited Pepsi bwana Promod  Nair( wadhamini wa kombe la meya Shinyanga 2015).

Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akiteta jambo na msimamizi wa kituo cha Shycom bwana Geofrey Tibakenda,na mratibu wa Kombe la Meya bwana Paul Mganga,ambaye ni mkurugenzi wa Myklay Entertainment(katikati). 

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post