|
Hapa ni katika ukumbi wa
mikutano wa Vijana Senta Ngokolo mjini Shinyanga ambako leo kumefanyika
kongamano la Vijana zaidi ya 13o kutoka mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na
wizara ya Afya na Ustawi kwa kushirikiana na kamati ya uendeshaji huduma za
afya mkoa wa Shinyanga.
Kongamano hilo lililenga kujadili changamoto mbalimbali
wanazokabiliana nazo vijana kuhusu suala la afya ya uzazi ikizingatiwa kuwa
mkoa wa Shinyanga ni mkoa unaoongoza kwa mimba na ndoa za utotoni.Mgeni rasmi
alikuwa kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Dkt Julius Thomas.
Vijana kutoka shule za
msingi na sekondari,vyuoni,mtaani,wazazi,viongozi wa madhehebu ya dini,na
wataalam mbalimbali kutoka mkoa wa Shinyanga.
Kongamano hilo pia limehudhuriwa
na Mratibu wa Afya ya Uzazi kwa Vijana kutoka wizara ya afya na ustawi
wa jamii nchini Dkt Elizabeth Kapella.
Malunde1 blog,ilikuwepo
eneo la tukio,mwandishi mkuu wa mtandao huu,bwana Kadama Malunde ametuletea
picha 38 kutoka eneo la tukio,Fuatilia hapa chini
|
|
Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Nuru Seni Muya akizungumza wakati wa kongamano hilo ambapo alisema suala la ukatili wa kijinsia,ndoa na mimba za utotoni bado ni changamoto kubwa mkoani Shinyanga |
|
Awali mratibu wa huduma
ya afya na uzazi na mtoto kutoka ofisi ya mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Joyce Kandolo amesema mkoa wa Shinyanga katika mikoa ya kanda ya ziwa ndiyo unaongoza
kwa mimba na ndoa za utotoni.
Kandoro ameongeza kuwa
takwimu zinaonesha kuwa vijana wengi chini ya miaka 19 wanafanya ngono huku
vijana wengi wa kike wakibainika kuwa ndiyo wenye maambukizi zaidi ya magonjwa
ya ngono na UKIMWI.
|
|
Mgeni rasmi
alikuwa kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Dkt Julius Thomas akizungumza katika kongamano hilo ambapo kilio cha Wadau wake wakiwemo
viongozi wa dini,vijana,wazazi,walimu na wanafunzi walisema asilimia kubwa ya
vijana wamekuwa wakipoteza ndoto zao kutokana na kujiingiza katika mahusiano
wakiwa na umri mdogo hali inayochangiwa na wazazi kutozungumza na watoto hao
juu ya afya ya uzazi.
|
|
Mratibu wa Afya ya Uzazi kwa Vijana kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii
nchini Dkt Elizabeth Kapella akizungumza katika kongamano hilo ambapo alisema jitihada za maksudi zinahitajika ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili vijana katika jamii
|
|
Kongamano linaendelea |
Mratibu wa Afya ya Uzazi kwa Vijanakutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii
nchini Dkt Elizabeth Kapella akisisitiza jambo
|
Wadau wakiwa ukumbini |
|
kongamano linaendelea |
|
Vijana wakiwa ukumbini |
|
Waandishi wa habari nao walikuwepo |
|
Meza kuu wakiteta jambo |
|
Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga
Charles Kisangure akichangia mawili matatu katika kongamano hilo la vijana.
|
|
Wadau wakiwa ukumbini |
|
Waigizaji
kutoka kundi la UMATI Entertainment Group wakiongozwa na mwigizaji maarufu
kutoka Bongo Movie Shinyanga Songoro Gadaffi wakitoa burudani katika kongamano
hilo la vijana.
|
Waigizaji
kutoka kundi la UMATI Entertainment Group wakiigiza kuhusu changamoto za afya
ya uzazi kwa vijana
Mwenyekiti wa taasisi ya
Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA) tawi la Shinyanga, Bw. Ezra Manjerenga
akizungumza katika kongamano hilo la vijana.
|
Mwenyekiti wa taasisi ya
Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA) tawi la Shinyanga, Bw. Ezra Manjerenga
akizungumza katika kongamano hilo la vijana ambapo alisisitiza umuhimu wa vijana kuwa tayari kuzungumzia matatizo yanawakabili ili kuyakabili
|
|
Mijadala katika makundi ikaendelea |
|
Wazazi wakiwa ukumbini |
|
Waandishi wa habari nao wakaendelea na mjadala juu ya changamoto za afya ya uzazi kwa vijana |
|
Walimu nao wakaendelea na mjadala |
|
Mijadala ikaendelea.... |
|
Vijana wanaendelea na mjadala |
|
Vijana wenye umri wa miaka kati ya 10 hadi 14
wakiwasilisha kazi ya kundi lao juu ya changamoto wanazokabiliana nazo kuhusu
afya ya uzazi.
|
|
Mwanafunzi
wa Chuo cha Muccos Kizumbi bwana Paschal akiwasilisha kazi ya kundi lake
|
|
Tunafuatilia kinachoendelea..... |
Kijana
Mohamed Mustapha kutoka mjini Shinyanga akiwasilisha kazi ya kundi lake
|
Vijana wakiwa ukumbini |
|
Ustadhi Fadhil Charamanda akizungumza wakati wa
kongamano hilo la Vijana.
|
|
Mtangazaji wa Radio Faraja bwana Faustine Kasala
akiwasilisha kazi iliyofanywa na kundi la waandishi wa habari kuhusu changamoto
wanazokabiliana nazo katika kuandika habari zinazohusiana na afya ya uzazi kwa
vijana.
|
|
Kongamano linaendelea... |
|
Mratibu wa Afya ya Uzazi kwa Vijana kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii
nchini Dkt Elizabeth Kapella akizungumza katika kongamano hilo |
|
Mratibu wa Afya ya Uzazi kwa Vijana kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii
nchini Dkt Elizabeth Kapella akizungumza katika kongamano hilo |
Kongamano linaendelea
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com