TAZAMA PICHA- WATANGAZAJI RADIO FARAJA,WATUMA SALAMU,M4D NA TYD PLAN WATOA MSAADA KWA WATOTO ALBINO BUHANGIJA


Hapa ni katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi(albino),wasioona na wasiosikia cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga ambapo leo Juni 06,2015 kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo ya Shinyanga inayomilikiwa na kanisa katoliki kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Watuma Salamu kwa njia ya Radio mkoani Shinyanga,Shirika la  Media For Development( M4D) na shirika la Tanzania Youth Development Plan( TYD Plan) wametoa misaada mbalimbali ikiwemo chakula na kupika chakula kwa ajili ya watoto hao.
Miongoni vitu walivyotoa ni Unga wa sembe,unga wa ngano,maharage,mafuta ya kupikia,sukari,chumvi,sabuni na mchele.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog ,Kadama Malunde,ametuletea picha 35 kutoka eneo la  tukio Tazama picha hapa chini

Mtangazaji wa Radio Faraja Jenifa Mahesa maarufu kwa jina la "Mama Mchungaji" akiendesha maombi maalumu katika kituo cha Walemavu wa ngozi cha Buhangija mjini Shinyanga leo

Mkuu wa kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Buhangija Peter Ajali akizungumza baada ya waandishi wa habari na watangazaji wa Radio Faraja na wadau wao walipotembelea kituo hicho.

Mwalimu Peter Ajali alisema Changamoto kubwa iliyopo katika kituo cha Buhangija ni Ukosefu wa Chakula kwa watot hao ambao sasa albino ni 292,wasioona 40 na wasiosikia 64.
Ajali alisema kutokana na changamoto ya Chakula hivi sasa Mlo mmoja pekee wa watoto hao unga ni kilo 60 hadi 70 na siku nzima wanatumia kilo 120 za unga na kwamba watoto hao hawana chakula kingine tofauti na ugali katika milo yao.

Wafanyakazi wa Radio Faraja na watuma salamu mkoani Shinyanga wakiwa eneo la tukio

Tunafuatilia kinachoendelea.....

Eneo la tukio
Mtangazaji wa kipindi cha Michapo ya Jioni kutoka radio Faraja Fm stereo,Bwana Steve Kanyefu maarufu kwa jina la Mwanaporii akiwa na mtoto mwenye albinism katika kituo cha Buhangija

Meneja msaidizi wa Radio Faraja ndugu Simeo Makoba akizungumza katika eneo la tukio.Makoba alisema pamoja na kazi kubwa wanayoifanya kuhamasisha jamii kujitokeza kuwasaidia watoto wenye ulemavu wa Buhangija na wazee wanaolelewa katika  kituo cha Kolandoto wameamua kufika katika kituo hicho ili kuwa mfano kwa jamii badala ya kutoa tu elimu kupitia chombo chao cha Habari wakishirikiana na shirika la TYD Plan,M4D na watuma salamu mkoani Shinyanga.

Watoto,watangazaji wa radio,watuma salamu wawakilishi wa mashirika ya TYD na M4D wakiwa eneo la tukio

Mkurugenzi wa shirika la TYD Plan Hans Alexander Msoka akizungumza katika eneo la tukio ambapo alisema wameguswa na maisha magumu wanayoishi watoto hao hivyo kuwaomba wadau wengine kufika katika kituo hicho ili kuwasaidia watoto hao wanaoishi maisha magumu
Eneo la tukio
Katibu Mwenezi wa Umoja wa Watuma Salamu mkoa wa Shinyanga Philemoni Mswanzari Masamaki akizungumza katika kituo hicho cha watoto wenye walemavu ambapo aliitaka jamii kuacha kuwafanyia ukatili albino.Masamaki alisema kauli mbiu ya Watuma Salamu ni “ Badili fikra kwa pamoja tutokomeze mauaji ya albino”

Mkurugenzi wa shirika la Media For Development Anikazi Kumbemba akizungumza katika kituo cha walemavu cha Buhangija ambapo aliitaka jamii kubadilika na kuacha kuamini kuwa viungo vya albino vinawapa utajiri na kufanikisha mambo yao na kusisitiza kuwa vitendo hivyo vinasababishwa na ujinga hivyo elimu bado inahitajika katika jamii.

Mtuma salamu maarufu nchini Tanzania Yusuph Hamis maarufu kwa jina la MR PHONE aka Mzee wa Check akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo aliitaka jamii kuachana na imani potofu za kuua albino na kuongeza kuwa mwezi huu atatoa Gunia moja la Mchele kwa ajili ya watoto wa Buhangija.

Mtuma Salamu ,bi Zainabu Issa maarufu kwa jina la Mamaa wa Mapozi akizungumza katika kituo cha walemavu cha Buhangija mjini Shinyanga.

eneo la tukio

Meneja msaidizi wa Radio Faraja,wakurugenzi wa mashirika ya M4D na TYD Plan,mwakilishi wa watuma salamu mkoa wa Shinyanga wakijiandaa kukabidhi msaada wa chakula na mahitaji mengine kwa ajili ya watoto wa Buhangija

Meneja msaidizi wa Radio Faraja Simeo Makoba akishikana mkono na mtoto Samwel Mapolu wakati wa kukabidhi msaada

Mkurugenzi wa shirika la Media For Development (M4D) Anikazi Kumbemba akishikana mkono na  akishikana mkono na mkuu wa kituo cha Buhangija Peter Ajali
Mkurugenzi wa shirika la Media For Development Anikazi Kumbemba akishikana mkono na watoto wa Buhangija

Zoezi la kukabidhi chakula linaendelea
Mtoto Tabu Mabula akiwashukuru watangazaji wa Radio Faraja na wadau walioambatana nao kutoa msaada wa chakula na mahitaji mengine muhimu.

Mtoto Samwel Mapolu akizungumza,ambapo aliyashukuru mashirika na watu binafsi kwa kuendelea kuwapa misaada kwani maisha yao yako mikononi mwao kutokana serikali haioni umuhimu wa kuwapangia bajeti badala yake sasa wanahangaika tu na kuishi kwa mashaka.
Watuma salamu nchini Tanzania Milembe Robert "Shangazi) kulia na Zainabu Issa"Mamaa wa Mapozi" kushoto ni Flora Chasama " Mama wa Furaha" wakikoroga uji kwa ajili ya kupika ugali wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija
Mtangazaji wa radio Faraja  Jenifa Gambaseni akiosha vyombo katika kituo cha walemavu cha Buhangija mjini Shinyanga.

Mtangazaji wa Radio Faraja Moshi Ndugulile akipika ugali katika kituo cha Buhangija

Meneja Msaidizi wa Radio Faraja Simeo Makoba( mwenye miwani katikati) akizungumza baada ya kumaliza zoezi la kukabidhi msaada wa chakula na mahitaji mengine muhimu katika kituo cha Buhangija

Mkuu wa kituo cha Buhangija Peter Ajali(kushoto) akiwaaga wadau hao wa maendeleo na kuwashukuru kwa kufika katika kituo chake

Watangazaji wa radio Faraja na watuma salamu katika pozi

Mtangazaji wa Radio Faraja fm Stereo Veronica Natalis (V2) akicheza na watoto wa Buhangija
Picha za kumbukumbu zikaendelea kupigwa 

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post