Viongozi wa Chadema wakimuokoa Askari Polisi Zakayo |
Vurugu zinaendelea |
Askari wa jeshi la
Polisi mkoani Geita Insepekta Zakayo amenusurika kuuawa baada ya
kupokea kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira kali kwenye
mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema
uliofanyika mjini Geita jana maeneo ya soko kuu la Geita.
Inaelezwa kuwa askari huyo ambaye alikuwa amevalia
kiraia alifika katika mkutano huo akiwa na simu ambayo alionekana muda wote
akirekodi kila kitu katika mkutano,na alikuwa akifanya hivyo kwa kificho.
Wakati akiendelea kurekodi mwenyekiti
wa Chadema mkoa wa Geita Alphonce Mawazo ,alipanda jukwaani na kumuona akiendelea kurekodi....akasema
"Maaskari tunawaheshimu sana ,tunajua
kwamba kuna baadhi mnaagizwa na wakubwa zenu kuja kurekodi vitu ambavyo
tunavizungumza ,sisi hatukatai mtu kurekodi,kama unataka kurekodi kwanini usije
sehemu ya wazi unafanya kwa kificho “alisema.
Kuna askari ambaye tunamfahamu kavaa
kiraia na helmenti nyekundu na yupo hapa anarekodi......"
Baada ya kusema
hayo wananchi walimvamia askari huyo na kuanza kumpiga ngumi maeneo
mbalimbali ya mwili wake hali ambayo ilisababisha askari huyo kupata
majeraha usoni na mkutano kuvurukika kwa muda wa dakika 5.
Aidha baada ya wananchi
kumvamia Askari huyo Mawazo aliagiza walinzi wa chama hicho maarufu
kama Red Briged kuwazuia wananchi wasiendelee kumpiga huku
akiwataka wananchi hao waache kumpiga Askari.
Hata hivyo wananchi hao hawakusikia ndipo Askari
wanchadema walipoamua kutumia nguvu kwa kuwatawanya wananchi na kufanikiwa
kumuokoa.
"Makanda mwacheni,msimpige makamanda,
Red Briged kamuokoeni huyo “alisema mawazo ambapo askari hao walienda kumuokoa
na muda mfupi gari ya jeshi la polisi ikiwa na askari wa
kikosi cha kutuliza ghasia na kumpakiza kisha
kwenda kituoni naye kituoni wakiwa na makamanda wa Chadema",alisema
Kaimu kamanda wa Jeshi la
Polisi Peter Kakamba alikili kutokea kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi
bado unaendelea wa kubaini waliofanya tukio hilo.
“Ni kweli kuna Askari wetu
amepigwa,lakini tunaendelea na uchunguzi wa kuwatafuta watu waliomshambulia
askari huyo na nitatolea ufafunizi kesho saaa 4:00 asubuhi".
Hata hivyo baada ya vurugu hizo
kuisha mkutano huo uliolenga kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi
kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura linalotarajia kuanza Juni 9 mwaka
huu mkoani humo uliendelea ,ambapo Mawazo alimlalamikia Mkurugenzi
wa Halmasahuri ya mji Margareth Nakainga kwa kuweka vituo vichache vya
kujiandikisha na kudai hali hiyo ni njama za CCM .
“Inashangaza mji wa Katoro
ulivyo mkubwa na watu wengi, lakini wameweka kituo kimoja cha kujiandikisha,hii
inaonyesha wengi hawatajiandikisha kwani wengi watatembea umbali mrefu
zaidi ya km 8,na walivyowajanja maeneo mengi ambayo chadema imeshinda
uchaguzi wa serikali za mitaa ndiko wamepeleka vituo vichache”alisema
Mawazo.
Pia alitoa angalizo kwa tume ya
uaNdikishaji kuwa makini kutatua tatizo hilo mapema ili yasitokea
machafuko kwani wananchi hawatakubali kuona wenzao wanandikishwa na
wengine kuachwa na kwamba utaungana nao kufanya maandamano makubwa
yasiyo kuwa na kikomo ili kupinga hujuma hizo.
Aidha katioka mkutano huo baadhi ya
watia nia wa kiti cha ubunge na udiwani jimbo la Geita mjini
walijitokeza rasmi na kutanga za nia yao ya kugombea nafasi
hizo katika jimbo hilo ambapo nafasi ya ubunge walijitokeza
saba na udiwani zaidi ya 10 na kuwaomba wananchi kuwaunga mkono ili
kulikomboa jimbo hilo.
Na Valence Robert-Malunde1 blog Geita
Social Plugin