Mtoto
mmoja Emmanuel Sandu miaka 15 aliyefariki mwaka 2002 akiwa na umri wa miaka 2
juzi aliwatia hofu wananchi wa Kata ya Idahina Wilayani Kahama Baada ya
kuonekana kijijini akiwa hai.
Tukio
hilo ambalo limevuta watu wengi kwenye ofisi ya serikali ya Kata ya Idahina
limehusishwa na imani za kishirikina kwa madai mtoto huyo alichukuliwa kwa
nguvu ya giza na kuwekwa msukule.
Afisa
Mtendaji wa Kata hiyo Isack Madale amesema baada ya mtoto huyo kuonekana wazazi
wake, Baba yake mzazi anaitwa Sandu Swila na mama yake Salu Lushugembe
walijitokeza na kumfahamu
Aidha
mama yake amesema mtoto huyo wakati anazaliwa mwaka 2000 alikuwa na ugonjwa wa
mchango hivyo walimchoma alama kwenye paji la uso ambayo wamemtambua kwa
kutumia alama hiyo.
Kufuatia
hali hiyo Madale amesema ofisi yake inawasiliana na polisi Wilaya kwa hatua
nyingine ingawa amesema kutokana na msongamano mkubwa wa watu kujaa ofisini
kwake kumuona mtoto huyo ameamua awape wazazi wake.
Mtoto huyo haongei lolote na amechakaa mwili wake na akiulizwa jina anatamka moja tu la Emmanuel hali ambayo inaonyesha alikuwa akiishi katika mazingira yasiyokuwa ya kibinadamu.
Social Plugin