Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Uchawi Kahama!! MTOTO ALIYEFARIKI MWAKA 2002 AONEKANA AKIWA HAI,HAONGEI KACHAKAA,ADAIWA KUWA MSUKULE

Mtoto mmoja Emmanuel Sandu miaka 15 aliyefariki mwaka 2002 akiwa na umri wa miaka 2 juzi aliwatia hofu wananchi wa Kata ya Idahina Wilayani Kahama Baada ya kuonekana  kijijini akiwa hai.

Tukio hilo ambalo limevuta watu wengi kwenye ofisi ya serikali ya Kata ya Idahina limehusishwa na imani za kishirikina kwa madai mtoto huyo alichukuliwa kwa nguvu ya giza na kuwekwa msukule.

Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Isack Madale amesema baada ya mtoto huyo kuonekana wazazi wake, Baba yake mzazi anaitwa Sandu Swila na mama yake Salu Lushugembe walijitokeza na kumfahamu

Aidha mama yake amesema mtoto huyo wakati anazaliwa mwaka 2000 alikuwa na ugonjwa wa mchango hivyo walimchoma alama kwenye paji la uso ambayo wamemtambua kwa kutumia alama hiyo.

Kufuatia hali hiyo Madale amesema ofisi yake inawasiliana na polisi Wilaya kwa hatua nyingine ingawa amesema kutokana na msongamano mkubwa wa watu kujaa ofisini kwake kumuona mtoto huyo ameamua awape wazazi wake.



Mtoto huyo haongei lolote na amechakaa mwili wake na akiulizwa jina anatamka moja tu la Emmanuel hali ambayo inaonyesha alikuwa akiishi katika mazingira yasiyokuwa ya kibinadamu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com