MJAMZITO aliyefahamika kwa jina la Rotha Bujiku, amejifungulia bafuni karibu na zahanati ya kijiji baada ya kudaiwa kufukuzwa na wauguzi waliokuwa zamu siku hiyo, kwa maelezo kuwa anajifungua kila mwaka.
Tukio
hilo lilitokea wilaya ya Maswa katika mkoa wa Simiyu juzi majira ya saa 2
asubuhi baada ya mjamzito huyo kufika katika zahanati hiyo kwa lengo la
kupata huduma ya kujifungulia kwa wataalamu.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililovuta umati wa watu, mjamzito
huyo alikataliwa kupokewa na muuguzi wa zamu aliyetajwa kwa jina la
Constansia John.
Ilielezwa
kuwa muuguzi huyo alikataa kumpokea kwa madai kuwa mjamzito huyo
alishapewa maelekezo tangu awali kuwa anatakiwa akajifungue katika
hospitali ya wilaya ya Maswa kwani amekuwa akizaa watoto kwa mfululizo.
Inaelezwa
kwamba, wakati Rotha akiugulia maumivu ya uchungu, muuguzi huyo
alimpigia simu ya mkononi Muuguzi Mkunga wa zahanati hiyo, Leticia
Kachumi kumjulisha hali hiyo na alipofika alitaka mjamzito huyo aondoke
katika eneo hilo na atafute usafiri ili aweze kufika katika hospitali ya
wilaya kama alivyoelekezwa katika siku za nyuma.
“Leticia
alipofika hapo zahanati baada ya kupigiwa simu na Constansia, licha ya
kumuona anaendelea kulalamika kutokana na uchungu alimwamuru aondoke
eneo hilo mara moja na atafute usafiri wa kumfikisha hospitali ya wilaya
iliyoko umbali wa kilomita 36, kwani walishamweleza kuwa amekuwa akizaa
mfululizo na hiyo ni mimba ya kumi na moja,” alisema shuhuda, Kundi Mageni.
Kutokana
na hali hiyo, mjamzito huyo alilazimika kuondoka zahanati hapo bila
msaada wowote na baada kufika karibu na nyumba iliyoko na zahanati hiyo,
alikwenda katika bafu la nyumba ya jirani ambalo halina sakafu na
kujifungulia humo na baadaye kusaidiwa na wasamaria wema waliosikia
sauti ya mtoto.
“Kwa
kweli huyu mama amejifungulia katika mazingira machafu na hatarishi kwa
afya yake na mtoto aliyemzaa. Kwa kweli hili ni tukio la kusikitisha.
Huwezi kuamini wauuguzi hao ambao ni wanawake kumtendea mwenzao ukatili
wa kiasi hiki,” alisema Pili Kidesela, Diwani wa kata ya Shishiyu (CCM).
Mganga
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dk Jonathan Budenu aliyefika katika eneo la
tukio muda mfupi baada ya kupata taarifa hizo, alisema kitendo
kilichofanywa na wauguzi hao ni kinyume cha maadili ya kazi yao na hivyo
ni lazima hatua kali za kinidhamu zichukuliwe kwa wote waliohusika.
Mwingine ajifungulia kichakani
Wakati
hayo yakitokea Maswa, mkoani Arusha binti mwenye umri wa miaka 17
alijikuta akijifungulia kichakani baada ya kuzidiwa uchungu wakati
akisubiri kuombewa kwenye mkutano wa dini uliofanyika Viwanja vya
Magereza, Kisongo nje kidogo na Jiji la Arusha.
Anna
Ngitoria, mkazi wa Endurimeti, wilayani Arumeru, alikuwa miongoni mwa
mamia ya wakazi wa Arusha, Kilimanjaro na vitongoji vyake waliokuwa
wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja huo wa magereza kwa ajili ya kile
kilichodaiwa kuwa ni maombi yaliyoandaliwa na kituo kimoja cha redio cha
jijini Arusha, Radio Safina.
Kwa
kawaida uongozi wa kituo hicho huandaa makongamano ya kila mwezi kwenye
uwanja huo wa Kisongo na kujumuisha mamia ya watu, wengi wao wakiwa ni
wanawake na wasichana ambao hupendelea kuhudhuria maombezi hayo kwa
matarajio tofauti.
Mikusanyiko
ya maombi ya ‘Radio Safina’ imekuwa ikikusanya watu wengi mithili ya
‘Kikombe cha Babu,’ ambacho nacho kilivuma sana miaka mitatu iliyopita
na tukio la msichana huyo kujifungua katika moja ya matukio hayo kimezua
hisia tofauti mjini hapa.
Akizungumza
katika hospitali ya Mount Meru ambapo amelazwa kwa sasa, binti huyo,
Anna amekiri kuwa alijifungua kabla ya wakati kwa sababu alikuwa na
ujauzito wa miezi saba tu.
Mtoto wake njiti sasa anahudumiwa katika wodi maalumu iliyopo hospitalini hapo na wauguzi wanasema anaendelea vizuri.
HATUA ILICHUKULIWA BAADA YA TUKIO HILO
SAKATA LA MAMA MJAMZITO, ROTHA BUJIKU KUTIMULIWA NA WATUMISHI WA ZAHANATI YA SHISHIYU WILAYA YA MASWA MKOA WA SIMIYU NA KISHA KUJIFUNGULIA KATIKA BAFU AMBALO LILIKUWA NA MAZINGIRA MABAYA LIMECHUKUA SURA MPYA BAADA YA MGANGA MKUU WA WILAYA DR JONATHAN BUDENU KUWAHAMISHA WATUMISHI WOTE WA ZAHANATI HIYO KAMA IFUATAVYO:
1.MGANGA MFAWIDHI WA ZAHANATI HIYO,Bw CHACHA AMEHAMISHIWA ZAHANATI YA BUGARAMA.
2.MUUGUZI,LETICIA KACHUMI AMEHAMISHIWA KITUO CHA AFYA MWASAYI.
3.MHUDUMU WA AFYA,COSTANSIA PAUL AMEHAMISHIWA ZAHANATI YA MAGEREZA MALYA.
SWALI LA KUJIULIZA ADHABU HIYO NDIYO INAWATOSHA BAADA YA KUKIUKA MAADILI YA KAZI NA KUFANYA UNYAMA HUO?
HATUA ILICHUKULIWA BAADA YA TUKIO HILO
SAKATA LA MAMA MJAMZITO, ROTHA BUJIKU KUTIMULIWA NA WATUMISHI WA ZAHANATI YA SHISHIYU WILAYA YA MASWA MKOA WA SIMIYU NA KISHA KUJIFUNGULIA KATIKA BAFU AMBALO LILIKUWA NA MAZINGIRA MABAYA LIMECHUKUA SURA MPYA BAADA YA MGANGA MKUU WA WILAYA DR JONATHAN BUDENU KUWAHAMISHA WATUMISHI WOTE WA ZAHANATI HIYO KAMA IFUATAVYO:
1.MGANGA MFAWIDHI WA ZAHANATI HIYO,Bw CHACHA AMEHAMISHIWA ZAHANATI YA BUGARAMA.
2.MUUGUZI,LETICIA KACHUMI AMEHAMISHIWA KITUO CHA AFYA MWASAYI.
3.MHUDUMU WA AFYA,COSTANSIA PAUL AMEHAMISHIWA ZAHANATI YA MAGEREZA MALYA.
SWALI LA KUJIULIZA ADHABU HIYO NDIYO INAWATOSHA BAADA YA KUKIUKA MAADILI YA KAZI NA KUFANYA UNYAMA HUO?
Social Plugin