Wanasayansi nchini Uingereza
wanasema kuwa wana ushahidi kwamba watoto wanaodanganya bila mtu
kugundua wana kumbukumbu nzuri ikilinganishwa na wale wasiodanganya.
Watafiti
katika chuo kikuu cha Sheffield kwa siri walichukua filamu ya watoto wa
umri wa miaka sita na saba wakifanya mtihani uliokuwa na majibu ambayo
yalikuwa yameandikwa nyuma ya zao.
Wale waliodanganya kuhusu kile waliochofanya walifanya vyema kutokana na uwezo wao kukumbuka walichofunzwa.
Mmoja
ya watafiti hao Elena Hoicka alisema kuwa sababu kuu ni kwamba wale
wanaodanganya hulazimika kukumbuka ukweli wote pamoja na uongo.
Social Plugin