Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

VIGOGO WA CHADEMA WA "MAJENEZA" WAHAMIA CCM

Tawi la misheni(majeneza)ambalo awali lilikuwa linamilikiwa na CHADEMA)na kupeperusha bendera za chama hicho,kwa sasa linapeperusha bendera za CCM kama linavyoonekana pichani baada ya viongozi wake kutimukia huko.  
Fundi ujenzi akitengeneza shina la wakereketwa wa ccm kwenye tawi hilo tayari kwa ufunguzi hapo kesho na mgeni rasmi ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa Leonard Bugomola ambaye atawapokea rasmi vijana hao kesho.
Aliyekuwa mgombea ujumbe wa chadema tawi la misheni Midium Mayombo akiwa ameshika kifimbo chenye nembo ya chama cha mapinduzi,kama anavyoonekana picha zote na Victor Bariety Geita -Malunde1 blog

Viongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEAMA)wa  lililokuwa tawi la misheni almaarufu ‘Majeneza’lililopo kata ya kalangalala  mjini Geita akiwemo  Mwenyekiti,katibu na mweka hazina pamoja na wajumbe wake wote wametangaza rasmi kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM),kwa madai ya kuchukizwa na timua timua inayoendelea ndani ya chama cha CHADEMA.

Tayari viongozi hao wamepokelewa na Ibrahim Juma Ibrahim mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Wilaya,na kesho wanatarajia kupokelewa rasmi na mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm taifa(MNEC)Leonald Bugomola.

Viongozi waliotangaza kukihama chama hicho na vyeo vyao kwenye mabano ni pamoja na Benjamin  Mateja(mwenyekiti)Ndoshi Ndoshi(katibu) na Midium Mayombo(mwekahazina)ambaye pia alikuwa mgombea wa ujumbe tawi hilo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika desemba mwaka jana.
Mbali na viongozi hao,wajumbe wengine wa tawi hilo waliotangaza rasmi kukihama chama hicho na kujiunga na CCM ni pamoja na Shedu Hamza,Mohamed Salum,Samweli Masheria,Daniel Yagole,Edson Gelephace,Venardy Aloyce na Peter Masala.

Wengine ni Rashid Salum,Emmanuel Makoye,Thomas Mpogomi,Richard Nzagamba,John Kayaga,Majaliwa Fabian,Abel Bulala,Khamis Joseph,Athuman Samson,Malunda Kira,na Bahati Samson.

Wakizungumzia na Malunde1 blog kwa nyakati tofauti,kwenye tawi hilo walidai kuwa,sababu kubwa ya kuamua kujiunga na chama cha mapinduzi CCM,wamechoshwa na timua timua inayoendelea kwenye chama chao ambapo wamebaini kuwa chama hicho kinaendeshwa kikabila na kwamba timua timua inayoendelea hivi sasa ni kuweka mtandao wa watu wao waliowapanga kushika nyazifa mbalimbali ukiwemo ubunge wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu.

‘’Chama chetu kimezidi kufukuza viongozi,na sisi tumechoka kuamua kuchaguliwa viongozi wanaowataka wao maana kama kimeshindwa kutatua migogoro ndani ya chama kikishika dola itakuwaje”alihoji Mateja aliyekuwa mwenyekiti wa tawi hilo na mwanachama hai wa chadema mwenye kadi namba 2542666 na kuongeza.

‘’Hili lilikuwa tawi la chadema na mimi nilikuwa mwenyekiti wa tawi hili na sisi tumeshirikiana na uongozi uliofukuzwa kuing’oa CCM hapa mjini na tukafanikiwa na sasa kimekuwa chama cha upinzani hususani kwenye halmashauri ya mji wa Geita kwa kuchangishana fedha ili tuifute ccm,leo tumefanikisha uongozi tuliouchagua unafukuzwa,hii siyo halali ni bora turudi CCM ambako hakuna mambo ya kikabila kama ilivyo kwenye chetu cha zamani’’.

Kwa upande wake Yogole aliyekuwa mgombea ujumbe mtaa wa misheni kupitia CHADEMA alidai kujiunga upinzani kwa bahati mbaya kama abilia awapo barabarani ambapo linapotokea gari lenye umbo na rangi nzuri hulazimika kuingia ukiamini ni chombo imara wakati mashine
yake ni mbovu na haiwezi kuwafikisha popote.

Mbali na kuipongeza CCM kwa uimara wake, viongozi hao walisema vyama vya upinzani havina sera ya kuwakomboa Watanzania bali viongozi wake wanataka kujinufaisha.

Bw. Nzagamba aliyekuwa mwanachama hai wa chadema kwa kadi namba,2352089  alisema ameamua kurudi CCM baada ya kubaini kuwa, CHADEMA kinaendekeza ukabila na ndiyo maana wanaofukuzwa kwa sasa ni wale wanaotoka kanda ya ziwa ili kuandaa mtandao wa watu wao ambao wamekwishawaweka kwa ajili ya kugombea ubunge.

‘’We fikilia mwanza uongozi wa mkoa umesimamishwa,shinyanga pia na Geita,na ukichunguza wale walioandaliwa na uongozi wa juu kwa ajili ya kuhakikisha wanakuwa wabunge ndiyo waanzilishi wa migogoro ndani ya chama lakini hawaguswi na wanaoguswa ni wale wasio na mtandao ndani ya chama,hii haikubaliki hata kidogo’’alisema Nzagamba
Aidha walidai kuwa,wanao mpango wa kufungua shina la wakereketwa wa CCM kwenye mtaa huo wa misheni(Majeneza)na tayari wamechagua uongozi wa muda wa tawi hilo chini ya mwenyekiti wake Benjamini Mateja,Richard Nzagamba(katibu)na Daniel Yogole mwekahazina.

Hata hivyo mbali na makada hao wa chadema kuwa na kadi za chama hicho zikionyesha ni wanachama hai,Katibu wa muda wa jimbo la Geita Ezekiel Mapesa alipoulizwa kuhusiana na wanachama wake kuhamia  CCM alidai hawatambui.

Na Victor Bariety-Malunde1 blog Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com