Simanzi
vilio na majonzi vimetanda katika viwanja vya bunge wakati mwili wa
aliyekuwa mbunge wa Ukonga Mh Eugene Mwaiposa ulipokuwa ukiwasili katika
viwanja vya bunge mjini Dodoma kwa ajili ya waheshimiwa wabunge na watu
mbalimbali kutoa heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kupelekwa
jijini Dar es Salaam kwa mazishi.
Mwili huo uliwasili ukitokea katika hospitali ya mkoa wa Dodoma
ulipokuwa umehifadhiwa ambapo akitoa salamu za bunge Mh Naibu spika Job
Ndugai amesema marehemu alikuwa ni miongoni mwa wabunge wa jimbo ambao
walikuwa ni mahiri.
Naye mchungaji Samweli Mshana kutoka katika kanisa la kiinjIli la
kilutheri dayosisi ya Dodoma amewataka wabunge kusimama katika imani zao
na kumtegemea mungu na siyo kujiingiza katika mambo ya kishirikina.
Akitoa shukrani za familia shemeji wa marehemu Bw Karim Mtambo
amesema wanashukuru kwa kila jambo lilofanyika ila jambo kuu wanaiomba
bunge katika kumuenzi marehemu watekeleze kwa vitendo yale aliyokuwa
akiyasimamia bungeni.
Baadhi ya wabunge akiwemo Mh Iddy Azzani na Mh Hilary Aeshi
wamesema marehemu alijitahidi kupinga ufisadi na hasa ubinafishwaji wa
shirika la usafiri UDA ambao ulifanyika bila ya kufuata taratibu huska
pia alikuwa nguzo muhimu katika kamati yake ya Tamisemi.
Mh Mwaiposa alikuwa mbunge wa jimbo la Ukonga (CCM) ambaye
alifariki dunia siku ya jumanne tarehe mbili kwa shinikizo la damu
nyumbani kwake mjini Dodoma eneo la Chaduru na ameacha mume na watoto
wawili.
Via>>ITV
Social Plugin