Akieleza baada ya kuachiwa na jeshi la polisi alipokuwa amewekwa
chini ya usalama kwa zaidi ya masaa matano, mwenyekiti wa uhamashishaji
Chadema kanda ya kati Bi. Jesca Kishoa, amesema anashangaa kuona mkuu wa
wilaya ya Iramba akiwakataza kufanya mikutano huku vyama vingine
vimekuwa vikifanya mikutano, jambo ambalo hastahili kufanya hivyo
kwa sababu yeye anatawala wananchi wenye vyama tofauti na siyo chama
kimoja.
Kwa upande wao wananchi wa wilaya ya Iramba wametupia lawama kwa
jeshi la polisi kuzuiA mikutano minne ya Chadema, pia kutumia nguvu
kutawanya watu kwa kuwamwagia maji ya kuwasha na kuwapiga mbomu ya
machozi.
Akiongea kwa simu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida Bwana
Thobias Sedoyeka amesema wao wanatekeleza amri ya mkuu wa wilaya ya
Iramba ya kupiga marufuku na kuzuia mikutano yoyote ya hadhara
ifanyike wilayani humo.
Via>>
Social Plugin