Zoezi
la uchukuaji fomu za kuwanaia urasi wa jamhuri ya mungano wa Tanzania
kwa awamu ya tano kupitia Chama Cha Mapinduzi umeanza rasmi mjini Dodoma
kwa makada wa chama hicho waliotangaza nia ya nafasi hiyo ya juu ya
uongozi wa Tanzania.
Mji wa Dodoma pamoja na viunga vyake umepambwa kwa rangi za kijani
na manjano za makada na wafuasi wa chama hicho ambao wamewasindikiza
wagombea wanao waunga mkono.
Zoezi hilo limeanza mapema majira ya saa
nne asubuhi, saa tano na saa kumi na moja jioni kwa wagombea wa nafasi
hiyo, kufika makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma, kuchukua fomu
tayari kwa zoezi la kutafuta wadhamini ili kuwaunga mkono kutoka
Tanzania bara visiwani.
Akiongea waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hizo,
mheshimiwa Steven Masatu Wasira amesema kuwa ana nia ya dhati ya
kuwatumikia wanannchi, kwa kusimamia ukuaji wa uchumi, kwa kufufua
viwanda na kuboresha kilimo ambacho ni tegemeo kubwa la ajila kwa
wananchi na kukomesha rushwa kubwa na ndogo, wakati wa kupata huduma
mbalimbali nchini.
Waliokwisha chukua fomu tayari ni Mheshimiwa Professa Mark
Mwandosya, Mheshimiwa Stiven Masatu Wasira, na balozi Amina Salumu Ally.
Wanaotarajiwa kuchukua fomu siku ya Alhamis ni mhesimiwa John Pombe
Magufuri, aliyeoneonekana viwanja hivyo akimalizia hatua za mwisho,
Mheshimiw Edward Lowasa, Mh: Frederick Sumaye, Mh:Amosi Robert
Siantemi, Mh:Mohamedi Gharib Bilal,na balozi Ally Karume.