Zaidi ya watu 90 wamefariki kutokana
na pombe iliokuwa na sumu katika mji wa India, Mumbai huku wengi
wengine wakiwa hospitalini.
Vifo vya kwanza viliripotiwa siku ya Jumatano.
Naibu
wa kamishna wa polisi katika mji huo amesema kuwa watu 150 waliokunywa
pombe hiyo iliotengezwa nyumbani katika mtaa mmoja wa mabanda.
Vifo vinavyosababishwa na pombe iliyo na sumu vimekuwa jambo la kawaida
nchini India ambapo pombe rahisi inayotengezwa nyumbani ni maarufu
miongoni mwa wakaazi wake walio maskini.
Social Plugin