CHAMA CHA MAPINDUZI
MCHAKATO, MKAKATI NA MWENENDO WA
KUFANIKISHA UCHAGUZI MKUU WA DOLA KWA NAFASI YA (RAIS, WABUNGE NA MADIWANI) KWA MWEZI OKTOBA, 2015 TANZANIA
IMEANDALIWA NA LT. MK MAGOVA (MST)
WA JWTZ NA CCM.
WA => “LYASA, IMAGE, KILOLO, IRINGA TANZANIA”
TAREHE 08 JUNI 2015
1.0 UTANGULINZI:
Tanzania
ni taifa lenye mfumo wa vyama vingi vya siasa kidemokrasia, kwa mujibu wa Katiba
ya (Jamhuri ya muungano wa Tanzania)
ya mwaka 1977 toleo la mwaka 1992 mpaka sasa 2015.
Mpaka
sasa kuna vyama vya siasa 20 ambavyo vimesajiliwa kisheria kwa mujibu wa Katiba
ya nchi na vyama vyote vilivyo na usajili wa kudumu wanayo haki ya kusimisha
wagombea (Urais, Wabunge na Madiwani) katika mchakato huu wa uchaguzi wa mwaka
huu wa Oktoba, 2015.
Watanzania
tuko huru kwa mujibu wa Katiba ya nchi, kugombea nafasi yeyote ya (Urais, Ubunge na Udiwani) kwa
kuzingatia sheria za Tume ya uchaguzi bila vurugu wala shari.Wagombea wote ni
lazima wazingatie Katiba na Kanuniya
Tume ya uchaguzi na sheria za nchi. Pia bila kuingilia shughuli za vyombo
vya Dola vya ulinzi na usalama (JWTZ,
JKT, POLICE, MAGEREZA, UHAMIAJI NA FIRE
BRIGED), wakati wa shughuli za uchaguzi na kuwaheshimu wapiga kura.
Vyombo
vya habari,ni vyombo muhimu sana kutoa habari juu ya mwenendo wa chaguzi. Pia
vyombo vya habari ni kupata habari toka kwa mihimili ya Dola na kupeleka habari
kwa wananchi, ili kutoa habari kwa wananchi kwa kutumia (TV, Radio na Magazeti)
ili kujua mchakato na mwenendo wa uchaguzi wa Rais,
Wabunge na Madiwani.
Waraka
huu waelimishwe wana CCM kwa vikao au mikutano ya ndani.
2.0 MCHAKATO, MKAKATI NA MWENENDO WA UCHAGUZI:
2.1 Kwa
mujibu wa Chama Cha Mapinduzi mchakato
na mkakati wa mwenendo wa uchaguzi huazia kwa wanachama wa CCM kwa kutoa kura
za maoni kwenye (Kata, Majimbo na
Wilaya) na vikao vya kuwajadili wagombeawote waliogombea Urais, Ubunge na Udiwani kwa mujibu wa (Katiba na Kanuni ya uchaguzi) ndani ya
CCM.
2.2 Vikao vya(Kamati
ya maadili, Kamati ya sekretarieti, Kamati ya siasa, Halmashuri kuu na Mkutano
mkuu) kwa ngazi ya Kata, Wilaya na
Mkoa kwa kuwajadili (Wbunge na
Madiwani) na kupendekeza kwenda ngazi za juu kwa uteuzi wa wagombea. Baada
ya kuteuliwa watapambana na wagombea wa vyama vya upizani, kwa kunadi (Itikadi, Sera, Malengo, Mipango na Ilani)
kwa kila Chama. Wananchi wataamua ni mgombea wa chama gani wanamtaka na
kumchagua.
2.3 Kwa
ngazi ya taifa kuna mchakato wavikao vya (Organazesheni,
Sekretarieti, Kamati kuu, Halmashuri kuu na Mkutano mkuu) kwa ngazi ya
taifa kwa kuwajadili wagombea Uraisbaada ya kudhaminiwa na wana CCM kwa
zaidi ya mikoa 25 kwa (Tanzania bara na Zanzibar). Ndipo vikao hupendekeza na
kuteua mgombea mmoja wa CCM kugombea Urais kwa kupambana na wagombea Urais na
vyama vya upizani. Wpiga kura watamchagua wanayemtaka kwa mujibu wa kukubalika
kwa (Itikadi,
Sera, Malengo, Mipango na Ilani) kwa Chama Cha Mapinduzi.
3.0 MAMBO YA KUZINGATI KWA WAGOMBEA WOTE WA (URAIS, UBUNGE
NAUDIWANI) KWA
CHAMA CHA MAPINDUZI:
3.1
Wananchi wakumbushwe mchakato wa
historia ya utawala wa Tanzania.
A. Tanzania ni taifa la muungano wan chi
za (Tanganyika na Zanzibar) ambazo
zote zilitawaliwa na wakoloni mbalimbali.
B. Tanganyika na Zanzibar kulikuwa
utawala wa kimila kwa kuongozwa na (Watemi,
Watwa na Machifu) tangu mwaka 800 hadi mwaka 1885, wakoloni. Wajerumani
walikuja mwaka 1880 na warabu waliingia
Zanzibar tarehe 25/08/1896.
C. Wananchi wazalendo wa Tnganyika
walipinga wakoloni wa Ujerumani chini ya utawala wa Karl Peters, vilianza vita
vya majimaji tangu tarehe 04/08/ 1905 hadi 1907 viliongozwa na Kinjikitile Bokero Ngwale kwa ukanda wa
Ngarambe Matumbi. Walipigana (Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani, Morogoro na
Iringa)
D. Vita kuu ya kwanza ya Dunia
walipigana tangu mwaka 1914 hadi mwaka 1918.
E. Vita kuu ya pili ya Dunia walipigana tangu
mwaka mwaka 1939 hadi 1945.
F. Tanganyika ilitawaliwa na Wajermani
tangu mwaka 1885 hadi mwaka 1919.
G. Waingereza walitawala tangu mwaka 1920 hadi
mwaka 1961.
3.2
Tanganyika kupata uhuru na Zinzibar
kufanya mapinduzi.
3.3
Mchakato
wa kujitawala watanzania, mpaka sasa ni juhudi za
wananchi wanzalendo wa kujitolea bila malipo mpaka sasa.
A. TANU ilipigania (haki, usawa, uhuru na kujitawala) tangu mwaka 1954 hadi mwaka
1961, mpaka sasa tunaishi kwa amani na utulivu.TANU iliongozwa na (Mwalimu Julius Kambarage Nyerere)
B.
ASPilipigania
(haki, usawa, uhuru na kujitawala)tangu
mwaka 1857 na kufanya mapinduzi Januari, 1964 wananchi wazalendo walijitolea
bila malipo kufanya mapinduzi dhidi ya utawala wa Sultan toka Oman.ASP
iliongozwa na (AbeidAmani Karume).
C. Kwa uongozi wa mwenyekiti wa TANU.Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
(Baba wa Taifa) na mwenyekiti wa ASP.Hayati Abeid Amani Karume. Walihamasisha
wananchi wa(Tanganyika na Zanzibar) kuungana
Aprili, 1964 na kuwa Tanzania hadi sasa.
D. Vyama vya siasa vya TANUnaASPni
vyama vilivyoandaa uimara wa CCM katika (kutawala, kuongoza na kusimamia kwa nidhamu vyombo vya
ulinzi usalama) kwa manufaa ya umma wa Tanzania.
E. CCM tangu kuanza kazi ya kutawala mwaka
1977 ni chama chenye historia katika ulimwengu kwa mambo yafutayo:-
1)
Kiliimarisha uchumi wa taifa katika sekta za (kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda, biashara na wajasiriamali)
2) Kiliimarisha na kusimamia vyombo vya (ulinzi na usalama)
kwa kulinda wananchi, mali na mipaka ya nchi(anga, maji na nchi kavu).
3) Kiliimarisha sekta za (elimu, afya, mawasilano, nishati, madini
na siasa)
4) Kufundisha wapigania uhuru wa nchi
mojawapo wa nchi za kusini mwa Afrika(Angola, Mozambiki, Zimbabwe, Namibia na Afrika Kusini)
ili kujitawala kidemokrasia. Makamanda na wapiganaji wa jeshi la JWTZ walikufamashuja 101kwa kusaidia Mozambiki na makaburi yako
Nambele Mtwara. Kwa hiyo wananchi wajue hitoria ya CCM juuya amani na utulivu.
5) CCM ilipigana vita vya Kagera (Tanzania na Uganda)
kwa kuvamiwa na majeshi ya Uganda kwa kuongozwa na Nduli Idd Amin tarehe 25,10/1978
na mapambano ya vita yalianza rasimi kuanzia (Miziro, Mtukula na Kakuto) tarehe 22/01/1979 hadi tarehe 25/07/1978. Hadi kuwakomboa
Waganda.
6) Daraja
la mto Kagera lilivunja tarehe 25/10/1978 na kujengwa hadi kukamilika tarehe 03/11/1978
na majeshi ya JWTZ yalianza kuvuka na kuanza mapambano.
7) Mojawapo
wa makamanda wa vita vya kung’oa utawala wa Dikteta Nduli Idd Amin wa Uganda ni
kama wafuatao:-
A. Mwalimu
Julius JK Nyerere alikuwa (Amiri Jeshi Mkuu) wa vita vya Kagera.
B. Abud
Jumbe Mwinyi alikuwa makamu wa kwanza wa Rais Tanzania
C. Rashid
Mfaume Kawawa alikuwa makamu wa pili wa Rais Tanzania.
D. Edward
Moringe Sokoine alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
E. Jeneral
Abdalah Twalipo Mkuu wa majeshi (JWTZ) wakati wa vita vya Kagera kati ya
(Tanzania na Uganda).
F. Jeneral
David Msuguli alikuwa Kamanda mkuu wa vita mstari wa mbele.
G. Brigedia
Silas Mayunga –Mti Mkavu alikuwa Brigedi Kommanda wa 206 KV kwa upande wa
Kakunyu kelekea Mbarara Uganda.
H. Brigedia
John Keats Walden alikuwa Brigedi Kommanda wa 207 KV Miziro kuelekea Masaka
Uganda .
I.
Brigedia Mwita Chacha Marwa—Kambale Mamba
alikuwa Brigedi Kommanda wa 208 KV upande wa Mtukula kuelekea Masaka Uganda.
J.
Kuna mafisa na wapiganaji walipigana vita vya
Kagera usiku na mchana kwa (ushupavu na ujasiri) na walikufa mashujaa 601
na kuzikwa Kaboya Bukoba Kagera, mpaka sasa familia za mashujaa hao wanaishi
kwaa shida.
K. Wananchi
waliandaliwa mafunzo ya Mgambo na JWTZili kwenda kupigana vita na majeshi
ya kivita toka Uganda.
4.0
MCHAKATO NA MWENENDO WA
VYAMA VYA SIASA TANZANIA:
4.1
Tanzania kuna mchakato wa historia wa
vyama vya siasa tangu mwaka 1977
mpakaSasa mwaka huu wa 2015, lakini CCM ina mchakato ufutao:-
A. Mwaka 1977 vyama vya TANU
na ASP
wanachama wa vyama hivyo walaamwua
kuunga na kuwa (CCM =>
CHAMA CHA MAPINDUZI) mpaka sasa ni chama tawala.
B. Lengo la kuungana CCM
na ASP
ilikuwa ni kuimarisha (upendo, umoja,
undugu,
mshikamano, uelewano, uzawa, uhuru, uzalendo na mahusiano
bora)
C. Kuimarisha masuala ya (amani, utulivu, ulinzi, usalama na kubinafasi).
D. Kulaani, kukemea na kupinga masuala
ya (siasa uchwara, udini, ukabila,
ubaguzi wa
rangi, ulevi wa
madaraka, rushwa, hongo na takrima).
4.2
Tangu mwaka 1977 kulikuwa na mfumo wa
chama kimoja tawalana kusimamia
vyombo vya ulinzi na usalama cha CCM
hadimwaka1992.Ulipoanza
mfumo wa
vyamavingi vya siasa
mpaka sasa.
A. CCM mwaka 1992 ilitoa maoni kwa wanachi
wapige kura kuwa na mfumo wa vyama vingi au uendelee mfumo wa chama kimoja.
B. Matokeo ya kura za maoni, wananchi
80% walitaka uendelee mfumo wa chama kimoja kutawala na wananchi 20% walitaka
mfumo wa vyama vingi vya siasa.
C. Mchakato wa vikao vya CCM vilianza
kujadili na kufanya upembuzi yakinifu ili kufikia muafaka. CCM ilimwita Mwalimu JK Nyerere (Baba wa Taifa)atoe
maoni yake juu ya maoni ya wananchi. Alisema kuwa,kwa mujibu wa haki ya
Demokrasia ni kwamba, wengi wape lakini kwa sasa duniani nchi nyingi kuna mfumo
wa vyama vingi.Tanzania haiwezi kujitenga na mataifa kiuchumi na kisiasa. Kwa
hiyo wananchi waelimishwe kuwe na mfumo wa vyama vingi vya siasa ili kuepukana
na vurugu za watu wachache katika taifa, amani
na utulivu ndani ya umma vitatoweka. Kwa hiyo wachache wanaopenda mfumo wa
vyama vingi wakubalike.
4.3
Chaguzi kuu chini ya mfumo wa vyama
vingi vya siasa tangu mwaka1995 hadi
uchaguzi wa mwaka 2010 ni kama ufutao:-
A. Uchaguzi wa mwaka 1995 CCM
kilipata 69% na vyama vya upizani walipata 31%, CCM kilishinda.
B. Uchaguzi wa mwaka 2000CCM
kilipata 71% na vyama vya upizani walipata 29%, CCM kilishinda.
C. Uchaguzi wa mwaka 2005 CCM
kilipata 82% na vyama vya upizani walipata 18%, CCM kilishinda.
D. Uchaguzi wa mwaka 2010 CCM
kilipata 61% na vyama vya upizani walipata 39%, CCMkilishinda.
4.4
Kwa
mchakato huo wa mwenedo wa uchaguzi mkuu wa Dola tangu mwaka 1995 hadi
2010 Chama Cha Mapinduzi kilishinda.
Je! Uchaguzi wa Oktoba,2015 ni chama kipi
kitashinda. Wana CCMni
kuwa makini na hakuna kugawanyika na kukisaliti Chama Cha
Mapinduzi.Isipokuwa kwa kaulimbiu ya
(umoja ni
ushindi) izingatiwe.
4.5
Ushindi
wa CCM kwa mwaka huu utatokana na kufanya
vikao vya ndani kwa kutumia
jumuiya za CCM(WAZAZI, UWT na UVCCM)
kuratibu takwimu za wapiga kura, wapenzi,
wakerketwa na washabiki
wa CCM. Bila hivyo uchaguzi ni kulikoni ni lazima CCM kuwa
imara kwa kampeni.
5.0
CCM NI KUWA NA DHANA YA
(UKWELI NA UWAZI)
5.1
Wajibu
wa wagombea wa ngazi zote ni kueleza ukweli juu ya mapungu, matatizo, shida,
malalamiko na kero kwa
wananchi (wakulima, wafugaji na wavuvi)
wapewe maeneo ya
kufanyia shughuli zao za kilimo, mifugo na uvuvi. Siyo
kuwanyang’anya maeneo yao na
kupewa wageni.
5.2
Wagombea kuwaeleza (wafanya biashara, wajasilia mali, mama lishe,machinga,
bodaboda, wasafirishaji wa ndege, meli, magari
ya maroli na mabasi, mafuta, maji,
umeme, mawasiliano, na biashara nyingine) wazingatie
sheria, za kulipa kodi na
kupewa maeneo ya
biashara.
5.3
Wagombea kuwaambia haki zao (watumishi,
wafanyakazi, walimu, madaktari, majeshi,
wastaafu, wazee, walemavu, wanawake wenye mimba, watoto,
vijana kupata ajira,
matibau na dawa kuwa na ubora)
5.4
Wagombea kuwaeleza ukweli juu ya tuhuma zilizojitokeza juu ya wizi wa
fedha za
wananchi(ESCROW, ITPL, RUSHWA WIZI na EPA) licha watuhumiwa kesi zao
ziko
mahakamani na vyombo vya
sheria.
5.5
Wananchi wawe makini sana kuwachagua viongozi ambao si waadilifu, pia
viongozi wa
TAMISEMI kuratibu takwimu mbalimbali za(wazee, wanaume,
wanawake, walemavu,
watoto,
vijana, vifaa vya usafiri, zana za kilimo, ukubwa wa maeneo, mifugo, makazi,
kaya,
idadi ya shule, vituo vya afya, zahanati, haspitali, mashamba, na miundombinu
mbalimbali)
kwa Tanzania uchumi
mkubwa uko vijijini ambako kuna watu wengi sana.
5.6
Suala
la uwajibikaji juu ya (usawa,
haki za binadamu na utawala bora) ni jukumu la
mihimili ya Dola (Serikali kuu,
Bunge na Mahakama) kutenda haki kwa wananchi.
Mihimili ya Dola siyo
kutuhumiana na kashifa, hasa wakiwa bungeni, huo si utawala
bora ila ni ukiukaji wa
maudhui na maadili katika taifa letu.
5.7
Wananchi
wawe makini kuwachagua viongozi watakaokuwa makini juu ya kusimamia
mazingira na matibabu
kwenye vituo vya afya na hospitali pia kunakuwa na dawa za
kutosha, ambazo zina
kiwango chenye ubora. Pia viongozi watakaochaguliwa wawe
makini sana juu ya bidhaa
feki zinazoingizwa kwa njia za panya.
5.8
Viongozi
na watendaji waache masuala ya dhuluma na kutotenda haki kuwalipa watu
sitahil zao iwapo fedha
zitatolewa na serikali kwa shughuli za maendeleo ya jamii,
malipo ya safari na
uhamisho au malipo kwenye matibabu.
5.9
Wananchi
wawachague viongozi watakaosimamia haki za mahakama kuhukumu
mapema watu wenye makosa
ya jinai, kuliko watu kulundikana mahabusu zaidi ya miaka
mitano bila kuhukumiwa,
serikali inazidi kujenga Magereza kwa gharama.
A. MWISHO WANANCHI WAAMBIWE KWAMBA:-
B. Serikali ni wananchi au umma ndio
wanaolipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
C. Hazina na BoT ni haki ya wananchi
ambao hulipa kodi na VAT si haki ya mihimili ya Dola, fedha ni kwa ajili ya maendeleo
na kujenga miundombinu mbalimbali kwa wananchi.
D. Wananchi waambiwe kwamba(nchi na watu ni taifa) bila nchi na watu
hakuna taifa. Kwa sasa kuna baadhi ya viongozi na watendaji hawajali kusimamia
taifa katika masuala ya maendeleo, kwa manufaa ya taifa.
E. Wananchi wawe makini kuangalia mali
asili kama vile (wanyama,
misitu, ndege, madini, maji na mazingira) ni jukumu la wananchi
sehemu zao hasa vijini.
F. Wananchi wawe makini kwa wagombea
wanaotoa rushwa, hongo na takrima hawana sifa ya kuwaongoza wananchi katika taifa
letu ila wana sifa ya kuhujumu uchumi.
G. Wananchi wawe huru kuchagua kiongozi
anayekuwa karibu na wanachi kwa kusikiliza na kupokea kero zao na ushauri wakati wote siyo viongozi wa kushinda kwenye
Baa hafai.
H. Watanzana wote wajue kwamba, amani (haicheziwi,
haikosewi na haijaribiwa) kwani amani ikitoweka ni (majuto, kufa,
kuhangaika na kuimbia nchi yako) watu wote ni (kufikiri,
kutafakari na chambua) nini maana ya (usawa, uhuru, uzalendo, demokrasia, kubinafasi, haki za
binadamu na utawala bora) katika taifa letu la Tanzania vitazingatiwa.
+Kaulimbiu yetu tunahitaji (amani, siri, miiko, utulivu, upendo, mshikamano, umoja, uelewano,
kukubaliana, ulinzi na usalama)ni kuzingatia wakati wa uchaguzi bila vurugu wala shari+
--------------------------------------------
Lt Mberito Kimvelye Magova (mst)
(MBEKIMA)
KADA WA ELIMU YA JAMMI
=MUNGU
IBARIKI TANZANIA, AFRIKA NA ULIMWENGU KWA UJUMLA=
Social Plugin