Kuna wakati watu wengine sio kwamba
hawapendi watalii au hawapendi utalii kwenye nchi yao, Utalii unakuja na
vingi ikiwemo utamaduni mgeni.. Ukiwa maeneo ya Beach hivi kukutana na
Watalii wakiwa na nguo ndogo ndogo (za ndani) huku wakipunga upepo ni kawaida tu,
lakini kwa wengine hiyo sio sawa!!
Watalii wanne wamejikuta wakiingia
kwenye Headlines za vyombo vikubwa vya Habari Duniani kama Sky News, BBC
na CNN.. ishu ni kitendo cha Watalii hao kuvua nguo wakati wanatalii
juu ya Mlima Kinabalu ulioko Malaysia, alafu wakapiga picha wakiwa hawajavaa nguo kabisa !!
Mwongozaji wa Watalii hao aliwaambia
lakini kwamba ishu ya kuvua nguo sio poa kabisa kwa Malaysia na Sheria
zao, majibu yao hayakuwa mazuri>>> “shut up” and “go to hell“.
Jamaa hao walianza kama utani yaani
kutaniana nani ataweza kuvua nguo alafu wapige picha, matokeo yake wote
wanne wakavua.. Mitandao ikakuza story mwisho wake kesi yao inaendelea
Mahakamani.
Social Plugin