Hii sio mara ya kwanza kupata stori
kutoka Kenya kuhusu pombe ya kienyeji kuua watu, imeingia kwenye
headlines tena leo June 24 2015 ambapo watu saba wamefariki na wengine
wamelazwa Hospitali baada ya kunywa na pombe ya kienyeji.
Baada ya kunywa pombe hiyo walianza
kutetemeka na wengine wakashindwa kutembea, hii ikafanya watu wa Usalama
kuingia mtaa mmoja baada ya mwingine katika Kaunti ya Kiambu, Kenya.
“Macho yalianza kuuma, nikaanza kuumwa na tumbo” >>> aliongea mmoja watu waliokunywa Pombe hiyo na kuzidiwa.
Mtu mwingine nae anasimulia; “Nilivyokunywa nilijisikia tu ulevi wa kawaida, baadae usiku nikajisikia kutetemeka”
Watu hao walikutwa wakiwa na hali mbaya pembeni ya barabara.
Social Plugin