Mshukiwa wa mauaji ya watu tisa katika kanisa moja la kihistoria mjini Carolina Kusini amekamatwa.
Kulingana
na mwanasheria mkuu Lorreta Lynch,awali maafisa walimtaja kijana huyo
wa miaka 21 kuwa Dylann Storm kama mtu waliyekuwa wakimsaka kwa
shambulizi la Charleston.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa mshukiwa huyo aliyejihami na bunduki
aliketi katika mkutano wa mafundisho ya biblia kwa takriban saa moja
kabla ya kufyatua risasi na kuwaua wanawake sita na wanaume watatu
akiwemo mchungaji wa kanisa hilo. Maafisa wamelitaja shambulizi hilo kama la uhalifu wa chuki. Bi Lynch amesema idara ya haki itaangazia maswala yote ili kubaini njia mwafaka ya kumfungulia mashtaka mshukiwa.
Via>>BBC |
Social Plugin