Kuna baadhi ya nchi kama China wana
desturi ya kula nyama ya mbwa hata baadhi ya makabila ya hapa Tanzania
inadaiwa hutumia nyama ya mbwa kama kitoweo.
Pamoja na ulaji huo ambao wengi wao wanaamini hauna madhara, kuna taarifa kutoka Nigeria
zinazohusisha watu watano kupoteza maisha baada ya kudaiwa kula nyama
hiyo wakiwa katika hoteli moja ambayo ni maarufu kwa ulaji wa nyama ya
mbwa.
Brain Ogbondah ambaye
ni mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema watu hao waliripotiwa kufa
ikiwa ni muda mchache baada ya kula nyama hiyo iliyoandaliwa na Friday Dickson.
Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea na viongozi wa familia wamewataka watu kuacha kula nyama hiyo.
Social Plugin