|
Mchezo
wa Hisani kati ya wakongwe wa soka wa Timu
ya Simba na Yanga ulioandaliwa na taasisi ya Mzalendo Foundation kwa lengo la kupata
pesa kusaidia watoto wenye ulemavu wa ngozi(albino) katika kituo cha Buhangija
kilichopo katika manispaa ya Shinyanga umefanyika jana jioni katika Uwanja wa
CCM Kambarage mjini Shinyanga kwa maveterani wa Yanga kuibamiza Simba Veterani
bao 3-2. Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
|
Yanga Veterani walijipatia bao la kwanza katika dakika ya
pili kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji wao Deo Lukasi na katika dakika 21
Ally Yusuph akaiongezea Yanga bao la pili.
Katika dakika ya 17 kipindi cha pili Simba Veterani
wakajipatia bao la kwanza kupitia kwa Shauri Idd na dakika ya 19 kipindi cha
pili Deo Lukasi wa Yanga Veterani akaongeza bao la tatu na katika dakika ya 23
kipindi cha pili Monja Liseki akaipatia Simba bao la pili.
|
Watoto wenye ulemavu wa ngozi kutoka kituo cha Buhangija wakiangalia mechi kati ya Yanga Veterani na Simba Veterani katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga |
|
Mashabiki
wa soka mkoa wa Shinyanga wakiangalia mpambano huo ambao haukuwa na kiingilio
bali mchango wowote kuanzia shilingi elfu moja kwa ajili ya kuwasaidia watoto
wenye ulemavu wa ngozi katika kituo cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga. |
|
Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika uwanja wa CCM Kambarage |
|
Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika uwanja wa Kambarage |
|
Wachezaji wa Simba Veterani wakiwa na baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi
wanaolelewa katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga.
|
|
Wachezaji wa Yanga Veterani wakiwa na baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi
wanaolelewa katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga.
|
|
Wachezaji wa Yanga Veterani wakiwa na baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi
wanaolelewa katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga.
|
|
Mwenyekiti
wa taasisi ya Mzalendo Foundation inayojihusisha na Utawala Bora,Haki za
binadamu,utamaduni na michezo Khamis Mgeja akiwa na waamuzi wa mchezo huo pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM |
|
Mwenyekiti
wa taasisi ya Mzalendo Foundation inayojihusisha na Utawala Bora,Haki za
binadamu,utamaduni na michezo Khamis Mgeja akiwa na waamuzi wa mchezo huo pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM na watoto wenye ulemavu wa ngozi kutoka kituo cha Buhangija |
|
Mwenyekiti
wa taasisi ya Mzalendo Foundation inayojihusisha na Utawala Bora,Haki za
binadamu,utamaduni na michezo Khamis Mgeja akizungumza katika uwanja wa CCM
Kambarage ambapo alisema taasisi yake imeandaa mchezo huo ili kupata pesa kwa
ajili ya kununua mahitaji wanayohitaji watoto wenye ulemavu wa ngozi katika
kituo cha Buhangija. |
Mgeja alisema pesa zote zilizopatikana katika mchezo huo
zitakuwa kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa ngozi katika kituo cha Buhangija.
|
Bwana
Peter Bubinza mkazi wa Shinyanga ambaye ni mlemavu wa ngozi akizungumza uwanjani ambapo aliwataka
watanzania kuachana na imani potofu kuwa viungo vya albino vinaleta utajiri
kwani ingekuwa ni kweli basi maalbino wote wangekuwa matajiri. |
|
Mc maarufu kutoka mkoa wa Shinyanga Ice akiwa na mshangaliaji wa Yanga . |
|
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin