Maelfu ya wakazi wa ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga leo wamejitokeza kuzika mwili wa aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na kada wa Chama Cha Mapinduzi (1995- 2005)Leonard Derefa (73) aliyefariki dunia Julai 09,2015 muda mfupi baada ya kutoka kujisaidia uwani,ambapo chanzo cha kifo chake ni Shinikizo la damu.
Mazishi yamefanyika leo mchana nyumbani kwake katika mtaa wa Mbuyuni katika kata ya Ndembezi mjini Shinyanga,ambapo kabla ya mazishi hayo mwili wake ulipelekwa katika kanisa la Katoliki la Mama Mwenye Huruma kwa ajili ya MIsa takatifu kuombea mwili wa marehemu iliyoongozwa na askofu wa Jimbo katoliki la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu.
Watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali,vyama vya siasa,viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini na watu mbalimbali wenye mapenzi mema.
Kutokana na maelfu ya watu kuhudhuria mazishi hayo,wengi walikosa nafasi ya kukaa katika sehemu iliyoandaliwa,wakati wa mazishi kila mtu akataka walau kubeba kiasi kidogo cha udongo,wengine wakalazimika kuchungulia tu nje ya fensi/ukuta na wengine kupanda juu ya miti na fensi ili kujionea kilichokuwa kinaendelea wakati wa mazishi ya kada huyo wa CCM ambaye hata nyumba yake imepakwa rangi ya kijani.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,bwana Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio,ametuletea picha 65,ANGALIA HAPA CHINI.
Ndani ya kanisa katoliki familia ya marehemu Leonard Derefa na wakazi wa Shinyanga
Waliokaa mbele ni Familia ya marehemu Leonard Derefa wakiwa kanisani
Misa takatifu ya kumwombea marehemu Leonard Derefa inaendelea
Misa takatifu ya kumwombea marehemu Leonard Derefa inaendelea
Askofu wa Jimbo katoliki la Shinyanga Liberatus Sangu akiongoza Misa Takatifu ya Kumwombea marehemu Leonard Derefa katika kanisa la Mama mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga Leo.
Maaskofu/siyo wa kanisa katoliki wakiwa kanisani
Misa takatifu ya kumwombea marehemu Leonard Derefa inaendelea
Waombolezaji wakiwa kanisani
Waombolezaji wakiwa kanisani
Mwenye nguo nyeusi ni Mwenyekiti wa Baraza Vijana Chadema taifa Patrobas Katambi akiwa kanisani.
Misa takatifu ya kumwombea marehemu Leonard Derefa inaendelea
Waombolezaji wakiwa kanisani
Waombolezaji wakiwa kanisani
Ndani ya kanisa katoliki Ngokolo
Mwandishi wa habari Marco Maduhu akifuatilia kilichokuwa kinajiri kanisani….
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akifuatilia kilichokuwa kinaendelea kanisani,kulia kwake ni aliyekuwa naibu meya wa manispaa ya Shinyanga,pia diwaniwa kata ya Ndembezi ndugu David Nkulila .
Padre Fabian Kushoka akitoa salamu za rambi rambi ambapo alisema marehemu Leonard Derefa alikuwa na mchango mkubwa katika kanisa.
Askofu wa Jimbo katoliki la Shinyanga Liberatus Sangu akimwombea marehemu Leonard Derefa wakati wa Misa takatifu ya kumwombea marehemu Leonard Derefa
Askofu wa Jimbo katoliki la Shinyanga Liberatus Sangu akimwombea marehemu Leonard Derefa
Askofu wa Jimbo katoliki la Shinyanga Liberatus Sangu akimwombea marehemu Leonard Derefa
Padre Joachim Mahona ambaye pia ni mkurugenzi wa Radio Faraja Fm Stereo akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Leonard Derefa.
Askofu wa kanisa la KKKT Shinyanga akitoa Emmanuel Makala akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Leonard Derefa
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa heshima zake za mwisho kwa aliyekuwa mbunge wa Shinyanga Mjini 1995-2005 Leonard Derefa,nyuma yake ni aliyekuwa naibu meya wa manispaa ya Shinyanga ndugu David Nkulila
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwapa mkono wa pole familia ya marehemu Leonard Derefa.
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Leonard Derefa wakiutoa katika kanisa la Ngokolo na kuupeleka nyumbani kwa marehemu.
Padre kiongozi John Kulwa akiongoza ibada ya mazishi nyumbani kwa marehemu Derefa
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu katika mtaa wa Mbuyuni,wengine waliishia kuchungulia tu kama unavyoona pichani
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu kulikofanyika mazishi
Nyumbani kwa marehemu
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu
Vijana wa CCM wakitoa heshima zao za mwisho kwa Gwaride Maalum
Vijana wa CCM wakitoa heshima zao za mwisho kwa Gwaride Maalum
Vijana wa CCM wakiweka mwili wa marehemu Kaburini
Padre John Kulwa akiendelea na ibada ya mazishi
Mapadre wanaweka udongo kaburini
Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele akiweka udongo katika kaburi la Leonard Derefa
Waombolezaji wakigombani kumzika mpendwa wao
Mwenyekiti wa mtaa wa Mbuyuni,Bwana Chief Abdallah Sube akiweka mchanga kwenye kaburi
Padre John Kulwa akiweka msalaba kwenye kaburni la marehemu Leonard Derefa
Mjane wa marehemu akiweka shada la maua kwenye kaburni
Watoto wa kiume wa marehemu na wake zao wakiweka mashada ya maua
Watoto wa kike wa marehemu na waume zao wakiweka mashada ya maua
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiteta jambo na mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele
Mjukuu wa Mwanaderefa bwana Chibura Makorongo baada ya kuweka shada la maua
Marafiki zake na marehemu wakiweka mashada ya maua
Ndugu Erasto Kwilasa ambaye ni mjumbe wa kamati ya siasa CCM mkoa wa Shinyanga akiweka shada la maua kwa niaba ya Chama chake
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akiweka shada la maua
Mwenyekiti wa mtaa Mbuyuni kata ya Ndembezi bwana Chief Abdallah Sube, kulia ni mwenyekiti wa mtaa wa Magadula kata ya Ngokolo bi Diana Ezekiel
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiweka shada la maua
Naibu waziri ofisi ya makamu wa rais pia mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele akiweka shada la maua juu ya kaburi la aliyekuwa mbunge wa Shinyanga Mjini mwaka 1995- 2005 Leonard Derefa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete
Naibu waziri ofisi ya makamu wa rais pia mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa mbunge wa Shinyanga Mjini mwaka 1995- 2015 Leonard Derefa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete
Aliyevaa nguo nyeusi ni mwenyekiti BAVICHA taifa ndugu Patrobas Katambi ,kulia kwake ni mbunge wa viti maalum CHADEMA mkoa wa Shinyanga ndugu Rachel Mashishanga wakiwa msibani kuwakilisha UKAWA
Waombolezaji wakiwa msibani
Waombolezaji wakiwa msibani
Waombolezaji wakiwa msibani
Mwenyekiti wa bodi ya afya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Wilson Majiji akitoa salamu za rambi rambi,Marehemu Derefa alikuwa mjumbe wa bodi hiyo hadi umauti unamfika
Mwenyekiti BAVICHA taifa ndugu Patrobas Katambi akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya UKAWA ambapo alisema mzee Derefa alikuwa mtu mwema asiyependa ubaguzi wa aina yoyote ndiyo maana hata watu waliojitokeza ni wengi sana kiashirio cha kwamba alikuwa mtu wa watu
Ndugu Erasto Kwilasa ambaye ni mjumbe wa kamati ya siasa CCM mkoa wa Shinyanga akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya Chama ambapo alisema CCM imepoteza kada muhimu kwani alipenda zaidi uwazi katika maisha yake
Waombolezaji wakiwa msibani
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ambapo alisema serikali inatambua mchango mkubwa marehemu Derefa huku akiiomba familia na jamii kwa ujumla kuna na subira katika kipindi hiki kigumu
Naibu waziri ofisi ya makamu wa rais pia mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete ambapo alisema chama cha Mapinduzi na serikali wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mzee Derefa na kwamba atakumbukwa kwa mambo mengi muhimu ya kujenga chama na serikali
Waombolezaji wakiwa msibani
Waombolezaji wakiwa katika geti la nyumba ya marehemu
Kulikuwa na maelfu ya waombolezaji,wengine hawakupata nafasi kukaa katika sehemu iliyoandaliwa,wakaamua kupanda juu ya uzio/geti na wengine kwenye miti ili kujua kilichokuwa kinaendelea wakati wa mazishi
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu,katika mtaa wa Mbuyuni kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog Shinyanga.
Malunde1 blog inawapa pole ndugu jamaa,na marafiki waliofikwa na msiba huo.Pumzika Kwa Amani mpendwa wetu Leonard Newe Derefa....
SOMA HAPA KUSOMA TAARIFA KAMILI KUHUSU KIFO CHA MWANA DEREFA
SOMA HAPA KUSOMA TAARIFA KAMILI KUHUSU KIFO CHA MWANA DEREFA
Social Plugin