Watia nia kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi( CCM) wameendelea kujitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea uongozi kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao ambapo leo Kijana Sinzo Khamis Mgeja(Kulia) mwenye taaluma ya ualimu amefika katika ofisi za CCM mkoa wa Shinyanga kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania ubunge wa viti maalumu kundi la Vijana mkoa wa Shinyanga.
Sinzo Khamis Mgeja ambaye ni mtoto wa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga ndugu Khamis Mgeja alifika katika ofisi hizo kuchukua fomu leo asubuhi Julai 17,2015 na mchana Julai 17,2015 akarudisha fomu hizo baada ya kufuata taratibu zote zinazotakiwa.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,bwana Kadama Malunde,ametuletea picha 10 ,ANGALIA HAPA CHINI
Julai 17,2015 asubuhi-Kushoto ni katibu wa UVCCM Teddy Athumani akimkabidhi Sinzo Khamis Mgeja fomu ya kuwania ubunge wa viti maalum kundi la vijana mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi,lengo likiwa ni kuwakilisha vijana wa mkoa wa Shinyanga Kulia ni Sinzo Khamis Mgeja ambaye ni mhamasishaji Vijana kata ya Nyanhembe wilayani Kahama na mjumbe wa Baraza la Vijana kata ya Nyanhembe akichukua fomu ya kuwania Ubunge Viti Maalum kundi la Vijana mkoa wa Shinyanga Sinzo Khamis Mgeja ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Chuo cha Mtakatifu Maria akionesha fomu ya kuwania ubunge Viti Maalumu kundi la Vijana mkoa wa Shinyanga kupitia CCM Julai 17,2015,Mchana-Sinzo Khamis Mgeja akirudisha fomu ya kugombea ubunge viti Maalumu kundi la Vijana mkoa wa Shinyanga,kushoto ni katibu muhtasi ofisi ya katibu wa UVCCM mkoa wa Shinyanga bi Regina Shija Sinzo Khamis Mgeja akirudisha fomu ya kugombea ubunge wa viti maalum kundi la vijana mkoa wa Shinyanga Sinzo Khamis Mgeja akisaini kitabu baada ya kurudisha fomu Sinzo Khamis Mgeja akiwa na mdogo wake Mariam Khamis Mgeja ndani ya ofisi ya CCM mkoa wa Shinyanga Sinzo Khamis Mgeja akiwa na mke wa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga /mama Mgeja(katikati) na Mariam Khamis Mgeja (kushoto) waliomsindikiza wakati wa kuchukua fomu ya kuwania ubunge wa viti Maalum kundi la vijana mkoa wa Shinyanga
Sinzo Khamis Mgeja akiwa na mke wa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga /mama Mgeja(katikati) na Mariam Khamis Mgeja (kushoto) .
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog Shinyanga
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin