Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA- MKUTANO WA CHADEMA LEO SHINYANGA,MZIMU WA SHELEMBI WAUNGURUMA CHAMAGUHA




Leo Jumapili Julai 05,2015 jioni kumefanyika mkutano wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo katika kata ya Chamaguha katika manispaa ya Shinyanga,mkutano ambao umeongozwa na mwenyekiti wa vijana Chadema Taifa Patrobas Katambi ambaye hivi sasa anajiita MZIMU WA SHELEMBI.


Mamia ya wakazi wa eneo la Chamaguha katika manispaa ya Shinyanga wamehudhuria mkutano huo uliolenga kutoa elimu ya uraia ,uliofanyika barabarani kutokana na kile kilichodaiwa kuwa hakuna uwanja wa Mikutano katika kata ya Chamaguha.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog


Mwenyekiti wa BAVICHA taifa Patrobas Katambi akisalimiana na mtia nia mwenzake kuwania Ubunge katika jimbo la Shinyanga mjini Zenna Gulam.

Mtia nia kuwania Ubunge katika jimbo la Shinyanga mjini Jimmy Luhende akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wakazi wa Chamaguha na Shinyanga kwa ujumla kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili muda wa kuchagua madiwani,wabunge na rais watumie fursa hiyo kufanya maamuzi sahihi ya kuchagua viongozi wa UKAWA watakaowaletea maendeleo.

Wakazi wa Shinyanga wakiwa pembezoni mwa barabara wakifuatilia mkutano wa Chadema


Mwenyekiti wa Baraza la Vijana katika wilaya ya Kishapu David Seni Jisandu akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema wakazi wa Shinyanga wanaendelea kupigika na maisha kutokana na kuendekeza viongozi mafisadi wa CCM ambao hutumia muda wa uchaguzi kuwahonga vitu kidogo.


Mwenyekiti wa BAVICHA taifa Patrobas Katambi(Mzimu wa Shelembi)akizungumza na wakazi wa Kata ya Chamaguha ambayo iko nyuma kimaendeleo kiasi kwamba hata uwanja wa mikutano hakuna.
Tunafuatilia kinachoendelea...

Akizungumza katika mkutano huo Katambi (Mzimu wa Shelembi) aliwataka watanzania kubadilika na kuacha kuchagua viongozi kwa ushabiki na badala yake wachague viongozi wenye kuwaletea maendeleo.

Katambi amesema viongozi wengi wa Chama Cha Mapinduzi wameshindwa kuwawaletea maendeleo wananchi hali ambayo inawafanya watanzania walio wengi kuishi maisha ya kubahatisha.

Wakazi wa Chamaguha wakifuatilia mkutano huo

Wakazi wa Chamaguha wakiwa eneo la mkutano



Mkutano unaendelea...



Mkutano unaendelea...

Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la mkutano


Mwenyekiti wa BAVICHA taifa Patrobas Katambi akitoa elimu ya uraia kuhusu katiba ya nchi


Mkazi wa Chamaguha akisoma kipengele katika katiba juu ya jukwaa akiwa na Mwenyekiti wa BAVICHA taifa Patrobas Katambi

Mwenyekiti wa BAVICHA taifa Patrobas akiondolewa eneo la mkutano baada ya kumaliza kuwahutubia wakazi wa Chamaguha,ambapo katika hali isiyokuwa ya kawaida vijana wa Shinyanga walisukuma gari lake hadi kwenye ofisi za CHADEMA mjini Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com