Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA- HAWA NDIYO VIONGOZI WAPYA WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA,MALUNDE ANG'AA UENYEKITI



Viongozi wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga waliomaliza muda wao wakijiuzuru nyadhifa zao kabla ya uchaguzi mkuu kupata viongozi wapya wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga(Shinyanga Press Club- SPC)



Msimamizi wa uchaguzi mkuu wa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga David Nkulila akizungumza jambo wakati wa uchaguzi leo mjini Shinyanga

Kulia ni mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga aliyemaliza muda wake Shija Felician akimpongeza mwenyekiti mpya wa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ndugu Kadama Malunde(aliyevaa suti) baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi leo

Mwenyekiti mpya wa SPC Kadama Malunde,ambaye ni mkurugezi wa Malunde1 blog akiwa na mwenyekiti aliyemaliza muda wake Shija Felician

Viongozi wapya wa SPC wakiwa meza kuu

Katibu mkuu mpya wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ndugu Stephen Wang'anyi akizungumza baada ya uchaguzi,kushoto ni mweka hazina aliyetetea kiti chake bi Stella Ibengwe


Baadhi ya viongozi wa SPC wakiwa katika picha ya pamoja.

**********
Klabu ya waaandishi wa habari mkoa wa Shinyanga(Shinyanga Press Club-SPC) leo imefanya uchaguzi mkuu wa viongozi wake watakaoiongoza klabu hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu, ambapo Kadama Malunde amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo.

Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo uliofanyika mjini Shinyanga David Nkulila amesema, Malunde amewashinda wagombea wenzake watatu ambao ni Patrick Mabula,Marco Mipawa na Greyson Kakuru.


Kadama Malunde ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania, Kahama FM na Mkurugenzi wa Malunde1 blog ambayo ni blogu Mwanachama wa Chama cha Blogu Tanzania (Tanzania Bloggers Network, TBN).

Nkulila amewataja viongozi wengine waliochaguliwa kuwa ni Stephen Wang’anyi akichaguliwa kuwa katibu mkuu, Shaaban Alei kuwa makamu mwenyekiti,Katibu msaidizi Ally Lytawi na mweka hazina ni Stella Ibengwe pamoja na kamati tendaji ya wajumbe watano.

Baada ya kutangaza matokeo hayo Nkulila amewataka wanachama wa klabu hiyo,kuachana na tofauti za uchaguzi na badala yake kushirikiana na viongozi waliowachaguliwa ili kuleta maendeleo na mabadiliko katika klabu hiyo.

Akiongea baada ya kutangazwa kwa washindi hao, mwenyekiti mpya wa klabu hiyo Malunde Kadama, ametoa shukrani kwa wanachama wote, huku akiahidi kutenda haki kwa kila kila mmoja na kuzingatia katiba ya chama katika utendaji wao.

Kwa upande wake mwenyekiti aliyemaliza muda wake Shija Felician amewataka viongozi wapya wa klabu hiyo kuendeleza misingi ya ushirikiano waliouacha na kuwasisitiza kufanya kazi kwa uwazi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com