Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya J4 Express Juma Mahende mkazi wa Nyakato jijini Mwanza kwa tuhuma za kuwaua wakazi wawili wa jijini humo kwa kutumia bastola usiku wa kuamkia leo katika eneo la Nyakato sokoni.
Marehemu hao wawili wametambuliwa kuwa ni Ally Mohamed Abeid mkazi wa Igoma na Claude Sikalwanda mkazi wa Nyasaka.
Wakizungumzia mauaji hayo kwa masikitiko makubwa huku wakibubujikwa na machozi, kaka wa marehemu Ally Mohamed Abeid aitwaye Ramadhan Mohamed Abeid pamoja na dada wa marehemu Claude, Bi. Aziza Steven Sikalwanda wamevitaka vyombo vya dola kuhakikisha vinatenda haki katika uchunguzi wa suala hilo.
Mjane wa marehemu Ally Mohamed Abeid, Bi. Dominata Gabriel pamoja na mmiliki wa nyumba aliyokuwa anaishi marehemu Ally Mohamed Abeid iliyoko eneo la Igoma Bw. Roger Rwegasira wanaeleza walivyopokea taarifa za kuuawa kwa watu hao.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Charles Mkumbo ameeleza mazingira ya vifo vya watu hao ambao wameuawa kwa kupigwa risasi kifuani huku pia akiwaonya baadhi ya wamiliki wa silaha kuacha tabia ya kuzitumia ovyo kinyume na sheria na utaratibu.
Via>>ITV
Social Plugin