Nicholaus Kashanga Azalia Mbwambo( 40) mjumbe wa serikali ya mtaa wa Nyakato,Kamanda wa jeshi la jadi Sungusungu na wakala wa UKAWA katika zoezi la kuandikisha wapiga kura, akiwa na mashine ya BVR Chumbani kwake waliyokuwa wanaitumia usiku kuandikisha kinyume cha sheria
Kadi 5 zikiwa tayari zimechapishwa
|
Kadi tano zilizokuwa zimechapishwa na mashine hiyo |
Nicholaus Kashanga Azalia Mbwambo( 40) mjumbe wa serikali ya mtaa wa Nyakato,Kamanda wa jeshi la jadi Sungusungu na wakala wa UKAWA katika zoezi la kuandikisha wapiga kura akiwa amepigwa butwaa baada ya vyombo vya usalama kufika eneo la tukio
Mashine ya BVR ikiwa kwenye chumba cha Nicolaus
Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya |
Jeshi la polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga limekamata mashine moja ya BVR ikitumika
kuandikisha wapiga kura saa tatu usiku nyumbani kwa mjumbe wa serikali wa mtaa
wa Nyakato wilayani humo Nicholaus Kashanga Azalia Mbwambo( 40) mjumbe wa serikali ya mtaa wa Nyakato,Kamanda wa jeshi la jadi Sungusungu na wakala wa UKAWA(Chadema) katika zoezi la kuandikisha wapiga kura.
Akizungumza leo na
waandishi wa Habari mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya amesema tukio
hilo limetokea jana majira ya saa tatu usiku katika mtaa wa Nyakato ambapo
mashine hiyo ilikutwa ikiwa inafanya kazi ya kuandikisha wapiga kura kinyume cha sheria.
Mpesya amesema kuwa
vyombo vya usalama wilayani humo vilipata taarifa kutoka kwa raia wema
ambazo zimewezesha kukamatwa kwa mashine hiyo pamoja na vitambulisho
vitano ambavyo tayari vilikuwa vimeshakamilika kuandikishwa.
Ameongeza katika
harakati za kukamata mashine hiyo pia wameweza kumkamata mhamiaji haramu
mmoja raia wa Burundi ambaye tayari alikuwa ameshaandikishwa na mashine
hiyo akiwa ndani ya nyumba ya mwenyekiti huyo wa mtaa.
Mpesya amesema jeshi la
Polisi wilayani humo linamshikilia kaimu afisa mtendaji wa kata ya
Nyasubi Lugina Misango, ambaye ndiye mwenye dhamana ya kusimamia mashine
hizo kwa kosa la kuruhusu mashine hiyo kutumika nyumbani kwa kiongozi wa serikali ya mtaa.
Katika hatua nyingine
Mpesya amewataka waandishi wa habari wanaotumiwa kukanusha taarifa hiyo,
kutambua kuwa ofisi yake ni mamlaka kamili ya serikali na kwamba
wasubiri hatua za kisheria kwani ushahidi wa kukamatwa kwa mashine hiyo
upo kituo cha polisi.
Tangu kuanza kwa zoezi
la uandikishaji wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura
wilayani humo hilo ndio tukio la kwanza la aina yake ambalo limevuta
hisia, na Mpesya amesema jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi.
Social Plugin