CHANZO CHA SOKO LA WAKULIMA MJINI KAHAMA KUTEKETEA KWA MOTO CHAJULIKANA
Tuesday, July 14, 2015
TAARIFA KUTOKA MJINI KAHAMA ZINASEMA KUWA SOKO LA MKULIMA WILAYANI HUMO LIMEUNGUA MOTO KATIKA BAADHI YA MAENEO USIKU WA KUAMKIA JANA.
KWA MUJIBU WA MASHUHUDA NA WAHANGA WAMESEMA KUWA MOTO HUO UMETOKEA USIKU WA KUAMKIA JANA KUFUATIA SHOTI YA UMEME ILIYOTOKEA KWENYE CHUMBA KIMOJA CHA DUKA.
KIKOSI CHA ZIMA MOTO WILAYANI HUMO KIMEFANIKIWA KUUDHIBITI MOTO HUO KWA KIASI KIKUBWA LICHA YA KUSEMA KUWA MIUNDO MBINU IMEKUWA KIKWAZO KIKUBWA CHA KUWEZA KUFIKA SEHEMU YENYE MOTO.
NAO BAADHI YA WAFANYABIASHARA WAMEIOMBA SERIKALI KUWASAIDIA MIKOPO KWANI AJALI HIYO IMESABABISHA MITAJI YAO KUKATA NA WENGINE WAKIWA BADO WANA MADENI KATIKA TAASISI ZA KIFEDHA.
WAFANYABIASHARA WAKIWA NJE YA SOKO HILO
NYANYA ZIKIWA ZIMEHARIBIKA KATIKA ENEO HILO.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin