Mkazi wa Busoka wilayani
Kahama Mulele Ramadhan (19) ambaye alikuwa dereva wa bodaboda ameuwawa
kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali tumbuni na mtu asiyefahamika
aliyekuwa na nia ya kumpora pikipiki.
Tukio hilo limetokea
jana majira ya saa 7 mchana katika barabara inayoelekea Kitwana ambapo
marehemu alikodiwa na mtu asiyefahamika katika kituo cha pikipiki
kilichopo mtaa wa Manzese na walipofika njiani mtu huyo alitekeleza
mauaji hayo.
Mashuhuda wa tukio hilo
wameiambia kahama fm kuwa wakati wa tukio hilo marehemu alipiga kelele
za kuomba msaada na ndipo watu walipojitokeza kumpa msaada, lakini
muuaji huyo akatokomea kusiko julikana.
Mganga mkuu wa hospitali
ya halmashauri ya mji wa kahama Dk. Bruno Minja amethibitisha kumpokea
Mulele akiwa majeruhi, lakini akifariki dunia majira ya saa 9 alasiri
wakati wakiwa katika harakati za kuokoa maisha yake.
Kamanda wa polisi mkoa
wa Shinyanga Justius Kamugisha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kuwa omba wananchi wa eneo hilo kutoa ushirikiano kwa polisi ili kuweza
kumkamata mtu huyo ambaye ametekeleza mauajia hayo.
Mwili wa marehemu Mulele
umehifadhiwa kwenye chimba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya
halmashauri ya mji wa Kahama, huku ukisubiri taratibu za mazishi kutoka
kwa ndugu wa marehemu.