Mheshimiwa Lucy Mayenga
Wanachama wa Umoja wa Wanawake CCM(UWT) mkoa wa Shinyanga waliojitokeza kugombea nafasi za ubunge viti maalum kati ya kumi waliojitokeza kuwania nafasi hiyo,Mheshimiwa Lucy Mayenga ameibuka mshindi wa kwanza kwa kupata kura 353 akifuatiwa na mheshimiwa Aza Hilal aliyepata kura 342 kati ya kura 440 zilizopigwa.
Katika uchaguzi huo mgombea kupitia kundi la Wafanyakazi aliyejitokeza ni mmoja pekee ambaye ni Dkt Flora Masakilija,kundi la watu wenye ulemavu pia alijitokeza mmoja Rehema Joshua ambao wote walipata kura za ndiyo 331
Mheshimiwa Aza Hilal
Social Plugin