Katibu wa Chama cha wachimbaji madini Mkoani Geita Golden Kainga akizungumza jambo kwenye mkutano huo wa wadau wa Afya katika kutekeleza azimio la nchi za Kusini mwa Afrika SADC la kuthibiti ugonjwa wa Kifua Kikuu-TB kwenye maeneo ya migodi Unaofanyika Hotel ya GoldCrest ya jijini Mwanza kujadili utafti uliofanyika mwaka jana katika migodi mine katika wilaya za Kahama na Geita
Washiriki wa mkutano wa wadau wa afya wakiwa kwenye picha ya pamoja
IMEELEZWA kuwa,sababu za Serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii kutopeleka huduma za afya ikiwemo kujenga kituo katika kijiji cha Mgusu kata ya mtakuja Wilayani Geita chenye wachimbaji 9,324 wasio rasmi wa madini mbali na kuwepo ongezeko kubwa la wagonjwa waliogundulika kuwa na TB ni kutokana na kijiji hicho kuwa haramu(hakijasajiliwa).
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa wilaya ya Geita,Dk.Noel Makuza juzi kwenye mkutano mkuu wa Wadau hao uliofanyika GoldCrest Hotel ya jijini Mwanza ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa azimio la nchi za Kusini mwa Afrika SADC la kuthibiti ugonjwa wa kifua kikuu kwenye maeneo ya Migodi.
Dk Makuza alisema kuwa,wameshindwa kupeleka huduma za afya kwenye kijiji hicho kutokana na kuwa haramu(hakijasajiliwa)na kwamba watafanya hivyo iwapo serikali itakisajili huku akidai kuwa,tayari serikali ipo kwenye mchakato wa kukisajili ili kiweze kupata huduma stahiki zinazotolewa na serikali ikiwemo huduma ya Afya.
''Ni kweli,kama mwezeshaji alivyosema,kwamba wakati wa utafiti wao walifika katika kijiji cha mgusu na wakakuta hakuna huduma za afya ambazo wakazi wa pale huzipata kwa kutembea umbali mrefu,hii inatokana na kijiji hicho nitumie neno ni haramu maana hakijasajiliwa hivyo huwezi kupeleka huduma kwenye kijiji ambacho ni haramu lakini kwa kuwa serikali ipo kwenye mchakato huo kikishasajiliwa tuitapeleka huduma hizo''alisema Dk Makuza
Dk Makuza alikuwa akichangia mada kuhusu utafiti uliowasilishwa na Mshauri wa Afya wa Mgodi wa ACCACIA Dk.Zumbe Musiba ambaye alidai kuwa,Watu 227 wameripotiwa kuugua ugonjwa wa Kifua Kikuu mwaka 2012/13 kwenye Maeneo ya Migodi ya wachimbaji wadogo katika wilaya za Kahama mkoani Shinyanga na Geita mkoani Geita.
Kwa mjibu wa Dk Musiba,utafti uliofanyika kwenye migodi ya Kalole na Mwaziba wilayani Kahama ulkibaini kuwa watu 54 walilipotiwa kuugua ugonjwa wa Kifua kikuu(TB)katika maeneo hayo.
Takwimu hizo zinatokana na Utafti ulifanywa Mwishoni mwa mwaka jana kwa kushirikisha wadau wa Afya likiwemo shirika la Kimataifa la Uhamiaji(Internation Organization For Migration -IOM),wachimbaji wadogo na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii..
Alisema watu hao wameripitiwa kuugua TB baada ya kufikishwa kwenye vituo vya Afya vya kata za Lunguya na Chela kupima Afya zao kutokana na kuishi katika migodi ambayo mazingira yake ni machafu yenye vumbi kali na matumizi ya zebaki bila kuwa na tahadhari.
Dk.Musiba alisema asilimia 50 ya kesi za Ugonjwa wa Kifua kikuu zilizoripotiwa katika maeneo hayo zina uhusiano mkubwa na Maambukizi ya Virusi vya Ugonjwa wa Ukimwi.
"Kati ya watu tuliowahoji,Utafti unaonyesha kuwa wengi hawajui dalili za TB hata viongozi wao hawajui dalili na chanzo cha Ugonjwa huo,Tumeona chanzo cha ugonjwa huo ni mwingiliano mkubwa wa watu,Vumbi linalotokana na uzalishaji wa mawe ya dhahabu,Nyumba finyu zisizopitisha hewa"alisema Dk.Musiba.
Aidha Mratibu wa mpango wa Taifa wa Kuthibiti Kifua Kikuu na Ukoma Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Dk.Alln Tarimo amesem katika Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi ya Gold Crest kwamba katika utafti uliofanyika Katika Migodi miwili ya Nyakagwe na Mgusu wilayani Geita unaonyesha watu 172 wameripotiwa kuugua TB.
Alisema katika Mgodi wa Nyakagwe watu 63 waligundulika kuwa na Ugonja wa TB Mwaka 2012 na mwaka 2013 walioripotiwa kuugua ugonjwa huo ni watu 62.
Dk.Tarimo aliongeza kuwa katika Mgodi wa Mgusu waliogundulika kuwa na TB mwaka 2012 ni watu 17,na idadi hiyo iliongezeka hadi kwa mwaka 2013 ambapo waliogungulika kuwa na ugonjwa huo ni watu 30.
Hata hivyo alifafanua kuwa pamoja na Nyakagwe kuwa na kituo cha Afya hakina huduma ya Kupima ugonjwa wa Kifua Kikuu na hivyo wanannchi hutembea umbali wa kilomita 25 kwenda kituo cha Afya Bukoli.
"Tulipofika Mgusu hapakuwa na kituo cha Afya wala huduma ya Vyoo hakuna hatua hiyo huwalazimu wananchi wa maeneo hayo kusafiri umbali wa kilomita 23 hadi 25 kwenda kupata tiba hiyo kwenye Hospitali ya wilaya ya Geita na Kituo cha Afya Nyankumbu"alisema Tarimo.
Kwa upande wake Naibu meneja wa mpango wa Taifa wa Kuthibiti kifua Kikuu Wizara ya Afya Dk.Liberate Mleoh,alisema Mpango huo unalenga kufikia malengo ya Taifa ya kuwa na wagonjwa sifuri wa TB ifikapo mwaka 2035 kutekeleza azimio la nchi za Kusini mwa Afrika SADC la kuthibiti ugonjwa huo kwenye maeneo ya Migodi.
Na Victor Bariety- Malunde1 blog Mwanza