Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KIKUNDI CHA WALIMU VIJANA CHA AMANI SHINYANGA ,CHATOA MSAADA WA CHAKULA KWA ALBINO KUSHEREKEA SIKUKUU YA EID EL FITRI



Katika kusherehekea sikukuu ya Eid El- Fitri leo kikundi cha Vijana Amani Group kinachoundwa na walimu wa shule za msingi wilaya ya kishapu,manispaa ya Shinyanga na Shinyanga Vijijini wametembelea kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi cha Buhangija mjini Shinyanga na kutoa zawadi/msaada wa chakula yakiwemo maharage Kilo 20,mchele kilo 70,mafuta ya kupikia lita 20 sabuni za kufulia maboksi mawili.

Mwenyekiti wa kikundi hicho cha Vijana Amani Group, Mwalimu Solo Lembe kutoka shule ya msingi Igegu Shinyanga vijijini, alisema wameona ni vyema kuwapelekea msaada huo wa chakula watoto hao ili na wao washeherekee kama watoto wengine wanaoishi na wazazi wao.

Mwandishi wa Malunde1 blog, Marco Maduhu alishuhudia tukio zima,ametuletea picha ,ANGALIA HAPA CHINI

Watoto wenye ulemavu wa ngozi wakiwa katika kituo cha Buhangija.Kituo cha Buhangija hivi sasa kina jumla ya watoto 404, ambapo changamoto kubwa ni uhaba wa chakula.

Walimu ambao ni wanakikundi cha Amani wakiwa katika kituo cha Buhangija

Wanachama wa Amani Group

Wanakikundi wa kikundi cha vijana amani Group kinachoundwa na baadhi ya walimu ya shule za msingi Kishapu ,Shinyanga manispaa na Shinyanga vijijini.

eneo la tukio

Wanakikundi cha Amani wakiwa na watoto wenye albinism leo katika kituo cha Buhangija

Mwalimu Jonathan Nathaniel kutoka Kishapu akikabidhi boksi la sabuni kwa watoto wenye albinism katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga


Mwalimu Jonathan Nathaniel kutoka Kishapu akikabidhi boksi la sabuni kwa watoto wenye albinism katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga

Eneo la tukio

Walimu wakiwa na watoto wenye albinism

Watoto wakipokea mafuta ya kupikia


Zoezi la utoaji zawadi linaendelea

Walimu wakiwa na watoto wa Buhangija

Watoto wakiwa eneo la tukio

Mtoto Mwajuma Mohamed akitoa shukrani kwa niaba ya watoto wenzake baada ya kupokea msaada wa chakula kutoka kwenye kikundi cha vijana amani Group kinachoundwa na baadhi ya walimu ya shule za msingi Kishapu ,Shinyanga manispaa na Shinyanga vijijini.

Kulia ni mwenyekiti wa kikundi hicho cha Vijana Amani Group, Mwalimu Solo Lembe kutoka shule ya msingi Igegu Shinyanga vijijini, akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo alisema wameona mi vyema kuwapelekea msaada huo wa chakula watoto hao ili na wao washeherekee kama watoto wengine wanaoishi na wazazi wao.



Mwajuma Mohamed alisema, kituo hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi kubwa zaidi ni uhaba wa chakula, hivyo wanawaomba wadau wa maendeleo kuendelea kuw saidia ili kuokoa maisha yao kutokana na kwamba asilimia kubwa hubebwa na wadau hao.kulia ni mwalimu Loyce Daudi ambaye ni mwalimu mlezi wa watoto hao.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde1 blog Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com