BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limeahirishwa ghafla leo baada
ya wabunge wa upinzani kusimama na kukataa kutoka nje ili kuzuia
miswada mitatu muhimu ya Gesi, Petroli na Uziduaji kusomwa kwa Hati ya
Dharura.
Hali hiyo imetokea baada ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika
kuomba mwongozo juu ya uvunjaji wa kanuni za bunge kwa kuwekwa miswada
mitatu sambamba.
Spika wa Bunge, Anne Makinda aliwataka wabunge hao kutoka nje kama
hawataki kuendelea na kikao ila baada ya kugoma kufanya hivyo na
kusimama kisha kuanza kupiga kelele, Spika aliamua kuahirisha bunge.
Miswada iliyowasilishwa ni hii hapa:
1.Muswada juu ya Petroli, 2015 (The Petroleum Act, 2015)
2.Muswada juu ya Usimamizi wa Mafuta na Gesi, 2015 (The Oil and Gas Revenues Management Act, 2015)
3.Muswada juu ya tasnia ya Uziduaji Tanzania (The Tanzania Extractive
Industries Act, 2015): The Tanzania Extractive Industries Act, 2015.
Social Plugin